Matthew 24:1-2
Kubomolewa Kwa Hekalu Kwatabiriwa
(Marko 13:1-2; Luka 21:5-6)
1Yesu akatoka Hekaluni na alipokuwa akienda zake, wanafunzi wake wakamwendea ili kumwonyesha majengo ya Hekalu. 2Ndipo Yesu akawauliza, “Je, mnayaona haya yote? Amin, nawaambia, hakuna hata jiwe moja hapa litakalobaki juu ya jingine, bali kila moja litabomolewa.”
Copyright information for
SwhNeno