‏ Matthew 24:3-14

Ishara Za Nyakati Za Mwisho

(Marko 13:3-23; Luka 21:7-24)

3Yesu alipokuwa ameketi kwenye Mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamjia faraghani, wakamuuliza, “Tuambie, mambo haya yatatukia lini, nayo dalili ya kuja kwako na ya mwisho wa dunia ni gani?”

4Yesu akawajibu, “Jihadharini, mtu yeyote asiwadanganye. 5Kwa maana wengi watakuja kwa Jina langu, wakidai, ‘Mimi ndiye Kristo,’
Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta.
nao watawadanganya wengi.
6Mtasikia habari za vita na matetesi ya vita. Angalieni msitishike, kwa maana haya hayana budi kutukia. Lakini ule mwisho bado. 7Taifa litainuka dhidi ya taifa, na ufalme dhidi ya ufalme. Kutakuwa na njaa na mitetemeko ya ardhi sehemu mbalimbali. 8Haya yote yatakuwa ndio mwanzo wa utungu.

9 “Ndipo mtasalitiwa, ili mteswe na kuuawa, nanyi mtachukiwa na mataifa yote kwa ajili yangu. 10Wakati huo, wengi wataacha imani yao, nao watasalitiana kila mmoja na mwenzake na kuchukiana. 11Watatokea manabii wengi wa uongo, nao watawadanganya watu wengi. 12Kwa sababu ya kuongezeka kwa uovu upendo wa watu wengi utapoa, 13lakini yule atakayevumilia hadi mwisho ataokolewa. 14Injili ya Ufalme itahubiriwa ulimwenguni kote kuwa ushuhuda kwa mataifa yote. Ndipo mwisho utakapokuja.
Copyright information for SwhNeno