‏ Matthew 24:45-51

Mfano Wa Mtumishi Mwaminifu

(Luka 12:41-48)

45 “Ni nani basi aliye mtumishi mwaminifu na mwenye busara, ambaye bwana wake amemweka kusimamia watumishi wengine katika nyumba yake, ili awape chakula chao kwa wakati unaofaa? 46Heri mtumishi yule ambaye bwana wake atakaporudi atamkuta akifanya hivyo. 47Amin, nawaambia, atamweka mtumishi huyo kuwa msimamizi wa mali yake yote. 48Lakini kama huyo mtumishi ni mwovu, naye akasema moyoni mwake, ‘Bwana wangu atakawia muda mrefu,’ 49kisha akaanza kuwapiga watumishi wenzake, na kula na kunywa pamoja na walevi. 50Basi bwana wa mtumishi huyo atakuja siku asiyodhani na saa asiyoijua. 51Atamkata vipande vipande na kumweka katika sehemu moja pamoja na wanafiki, mahali ambako kutakuwa ni kulia na kusaga meno.
Copyright information for SwhNeno