Matthew 26:14-16
Yuda Akubali Kumsaliti Yesu
(Marko 14:10-11; Luka 22:3-6)
14Kisha mmojawapo wa wale kumi na wawili, aitwaye Yuda Iskariote, alikwenda kwa viongozi wa makuhani 15na kuuliza, “Mtanipa nini nikimtia Yesu mikononi mwenu?” Wakamlipa vipande thelathini vya fedha. 16Tangu wakati huo Yuda akawa anatafuta wakati uliofaa wa kumsaliti Yesu.
Copyright information for
SwhNeno