Matthew 27:11-14
Yesu Mbele Ya Pilato
(Marko 15:2-15; Luka 23:3-25; Yohana 18:33–19:16)
11Wakati huo Yesu akiwa amesimama mbele ya mtawala, mtawala akamuuliza, “Wewe ndiye mfalme wa Wayahudi?” Yesu akasema, “Wewe wasema hivyo.” 12Lakini viongozi wa makuhani na wazee walipomshtaki, hakujibu neno. 13Ndipo Pilato akamuuliza, “Je, husikii ni mambo mangapi wanayokushtaki nayo?” 14Lakini Yesu hakumjibu hata kwa shtaka moja, kiasi kwamba mtawala alishangaa sana.
Copyright information for
SwhNeno