‏ Matthew 28:16-20

Yesu Awatuma Wanafunzi Wake

(Marko 16:14-18; Luka 24:36-49; Yohana 20:19-23; Matendo 1:6-8)

16Basi wale wanafunzi kumi na mmoja wakaenda hadi Galilaya kwenye ule mlima ambao Yesu alikuwa amewaagiza. 17Walipomwona, wakamwabudu; lakini baadhi yao wakaona shaka. 18Yesu akawajia na kusema, “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. 19Kwa sababu hii, enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, 20nanyi wafundisheni kuyashika mambo yote niliyowaamuru ninyi. Hakika mimi niko pamoja nanyi siku zote, hadi mwisho wa nyakati.”
Copyright information for SwhNeno