‏ Matthew 4:18-22

Yesu Awaita Wanafunzi Wake Wa Kwanza

(Marko 1:16-20; Luka 5:1-11)

18Yesu alipokuwa anatembea kando ya Bahari ya Galilaya, aliwaona ndugu wawili, Simoni aitwaye Petro, na Andrea ndugu yake. Walikuwa wakizitupa nyavu zao baharini kwa kuwa wao walikuwa wavuvi. 19Yesu akawaambia, “Njooni, nifuateni nami nitawafanya mwe wavuvi wa watu.” 20Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata.

21Alipoendelea mbele kutoka pale, akawaona ndugu wengine wawili, Yakobo mwana wa Zebedayo na Yohana nduguye, wakiwa wamekaa kwenye mashua pamoja na baba yao Zebedayo, wakizitengeneza nyavu zao. Yesu akawaita. 22Nao mara wakaiacha mashua yao, pamoja na baba yao, wakamfuata.
Copyright information for SwhNeno