‏ Matthew 8:14-15

Yesu Aponya Wengi

(Marko 1:29-34; Luka 4:38-41)

14Yesu alipoingia nyumbani kwa Petro, alimkuta mama mkwe wa Petro amelala kitandani, akiwa ana homa. 15Akamgusa mkono wake na homa ikamwacha, naye akainuka na kuanza kumhudumia.
Copyright information for SwhNeno