Psalms 40:13-17
13Ee Bwana, uwe radhi kuniokoa;Ee Bwana, njoo hima unisaidie.
14Wote wanaotafuta kuuondoa uhai wangu,
waaibishwe na kufadhaishwa;
wote wanaotamani kuangamizwa kwangu,
warudishwe nyuma kwa aibu.
15Wale waniambiao, “Aha! Aha!”
wafadhaishwe na iwe aibu yao.
16Lakini wote wakutafutao
washangilie na kukufurahia,
wale wapendao wokovu wako siku zote waseme,
“Bwana atukuzwe!”
17Lakini bado mimi ni maskini na mhitaji;
Bwana na anifikirie.
Wewe ndiwe msaada wangu na Mwokozi wangu;
Ee Mungu wangu, usikawie.
Copyright information for
SwhNeno