1 Chronicles 27

Vikosi Vya Jeshi

1Hii ndiyo orodha ya watu wa Waisraeli, viongozi wa jamaa, majemadari wa maelfu, majemadari wa mamia na maafisa wao, waliomtumikia mfalme kwa lo lote lile lililohusu vikosi vya jeshi vile vilivyokuwa zamu mwezi baada ya mwezi katika mwaka mzima. Kila kikosi kimoja kilikuwa na watu 24,000. 2

  • Msimamizi wa kikosi cha kwanza kwa mwezi wa kwanza, alikuwa Yeshobeamu mwana wa Zabdieli. Kulikuwa na watu 24,000 katika kikosi chake.
3Yeye alikuwa mzao wa Peresi na mkuu wa maafisa wote wa jeshi kwa mwezi wa kwanza. 4Msimamizi wa kikosi kwa mwezi wa pili alikuwa Dodai, Mhohi. Miklothi ndiye aliyekuwa kiongozi wa kikosi chake. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000. 5Jemadari wa kikosi cha tatu, kwa mwezi wa tatu, alikuwa Benaya mwana wa Yehoyada kuhani. Yeye ndiye aliyekuwa mkuu wa kikosi chake kilichokuwa na watu 24,000. 6Huyu ndiye yule Benaya aliyekuwa shujaa miongoni mwa wale Thelathini na ndiye aliyekuwa juu yao hao Thelathini. Mwanawe, Amizabadi, ndiye aliyekuwa mkuu katika kikosi chake. 7Jemadari wa nne, kwa mwezi wa nne, alikuwa Asaheli nduguye Yoabu, mwanawe Zebadia ndiye aliyeingia mahali pake kwenye uongozi. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000. 8Jemadari wa kikosi cha tano kwa mwezi wa tano alikuwa Shamhuthi, Mwizrahi. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000. 9Jemadari wa kikosi cha sita kwa mwezi wa sita, alikuwa Ira, mwana wa Ikeshi, Mtekoi. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000. 10Jemadari wa kikosi cha saba kwa mwezi wa saba, alikuwa Helesi, Mpeloni wa Waefraimu. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000. 11Jemadari wa nane kwa mwezi wa nane, alikuwa Sibekai, Mhushathi wa Wazera. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000. 12Jemadari wa tisa kwa mwezi wa tisa, alikuwa Abiezeri, Mwanathothi wa Wabenyamini. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000. 13Jemadari wa kumi kwa mwezi wa kumi alikuwa Maharai Mnetofathi wa Wazera. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000. 14Jemadari wa kumi na moja kwa mwezi wa kumi na moja, alikuwa Benaya, Mpirathoni wa Waefraimu. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000. 15Jemadari wa kumi na mbili kwa mwezi wa kumi na mbili, alikuwa Heldai, Mnetofathi, kutoka jamaa ya Othnieli. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000. Maafisa Wa Makabila 16
  • Maafisa waliokuwa wanaoongoza makabila ya Israeli walikuwa:
  • Kwa Wareubeni: Eliezeri mwana wa Zikri;
  • kwa Wasimeoni: Shefatia mwana wa Maaka;
17kwa Walawi: Hashabia mwana wa Kemueli; kwa Aroni: Sadoki; 18kwa Yuda: Elihu, nduguye Daudi; kwa Waisakari: Omri mwana wa Mikaeli; 19kwa Wazabuloni: Ishmaia mwana wa Obadia; kwa Wanaftali: Yerimothi mwana wa Azrieli; 20kwa Waefraimu: Hoshea mwana wa Azazia; kwa nusu ya kabila la Manase: Yoeli mwana wa Pedaya; 21kwa nusu nyingine ya kabila la Manase huko Gileadi: Ido mwana wa Zekaria; kwa Wabenyamini: Yaasieli mwana wa Abneri; 22kwa Wadani, Azareli mwana wa Yerohamu. Hao ndio waliokuwa maafisa wa kabila la Israeli. 23Daudi hakuwahesabu wale watu waliokuwa chini ya miaka ishirini, kwa sababu Mungu alikuwa ameahidi kuwafanya Israeli kuwa wengi kama nyota za angani. 24Yoabu mwana wa Seruya alianza kuwahesabu watu lakini hakumaliza. Kwa sababu ya kuwahesabu watu, hasira ya Mungu iliwaka juu ya Israeli, nayo hiyo hesabu yao haikuingizwa katika kitabu cha kumbukumbu za Mfalme Daudi.

Wasimamizi Wa Mali Za Mfalme

25Azmavethi mwana wa Adieli ndiye aliyekuwa msimamizi wa hazina za kifalme.

Msimamizi wa hazina katika mashamba, miji, vijiji na kwenye ngome alikuwa Yonathani mwana wa Uzia.

26Ezri mwana wa Kelubu alikuwa msimamizi wa wafanya kazi waliokuwa wanalima katika mashamba.

27Shimei, Mramathi, alikuwa msimamizi wa mashamba ya mizabibu.

Zabdi, Mshifmi, alikuwa msimamizi wa zabibu, utengenezaji na uhifadhi wa divai katika mapipa makubwa.

28Baal-Hanani, Mgederi, ndiye aliyekuwa mwangalizi wa mashamba ya mfalme ya mizeituni na mikuyu katika tambarare za vilima vya magharibi.

Yoashi alikuwa msimamizi wa ghala za mafuta ya zeituni.

29Shitrai, Msharoni, alikuwa msimamizi wa makundi ya ng'ombe waliojilisha huko Sharoni.

Shafati mwana wa Adlai alikuwa msimamizi wa yale makundi ya ng'ombe yaliyokuwa makondeni.

30Obili, Mwishmaeli, alikuwa msimamizi wa ngamia.

Yehdeya, Mmeronothi, alikuwa msimamizi wa punda.

31Yazizi, Mhagri, alikuwa msimamizi wa makundi ya kondoo na mbuzi.

Hawa wote ndio waliokuwa maafisa wasimamizi wa mali alizokuwa nazo Mfalme Daudi,

32Yonathani, mjomba wa Daudi, alikuwa mshauri, mtu mwenye ufahamu mkubwa na mwandishi. Yehieli mwana wa Hakmoni alikuwa akiwahudumia wana wa mfalme.

33Ahithofeli alikuwa mshauri wa mfalme.

Hushai, Mwarki, alikuwa rafiki wa mfalme.
34Baada ya Ahithofeli, Yehoyada mwana wa Benaya aliingia mahali pake kama mshauri wa mfalme pamoja na Abiathari.

Yoabu alikuwa ndiye jemadari wa majeshi ya mfalme.

Copyright information for Neno