1 Chronicles 9

Waisraeli wote waliorodheshwa katika koo zilizoandikwa kwenye kitabu cha wafalme wa Israeli.

Watu Katika Yerusalemu

Watu wa Yuda walichukuliwa mateka kwenda Babeli kwa sababu ya kukosa uaminifu kwa Mungu.
Basi watu wa kwanza kurudi kukaa kwenye milki zao katika miji yao walikuwa baadhi ya Waisraeli, makuhani, Walawi na Wanethini
9.2 Yaani wahudumu wa Hekalu
.

Wale waliotoka Yuda, Benyamini, Efraimu na Manase ambao waliishi Yerusalemu walikuwa:

Jamaa Za Yuda

 • Uthai mwana wa Amihudi, mwana wa Omri, mwana wa Imri, mwana wa Bani, wa wana wa Peresi, mwana wa Yuda.
Wazao wa Washiloni waliorudi ni: Asaya mzaliwa wa kwanza na wanawe. Kwa wana wa Zera: Yeueli. Watu wa Yuda jumla yao walikuwa watu 690. Jamaa Za Benyamini
 • Kwa Benyamini walikuwa:
 • Salu mwana wa Meshulamu, mwana wa Hodavia, mwana wa Hasenua;
Ibneya mwana wa Yerohamu, Ela mwana wa Uzi, mwana wa Mikri; na Meshulamu mwana wa Shefatia, mwana wa Reueli, mwana wa Ibniya. Watu kutoka Benyamini kama walivyoorodheshwa katika koo zao jumla yao ni 956. Watu hawa wote walikuwa viongozi wa jamaa zao. Jamaa Za Makuhani 10 
 • Wa jamaa za makuhani walikuwa:
 • Yedaya, Yehoyaribu na Yakini;
11 Azaria mwana wa Hilkia, mwana wa Meshulamu, mwana wa Sadoki, mwana wa Merayothi, mwana wa Ahitubu aliyekuwa afisa kiongozi wa nyumba ya Mungu. 12 Adaia mwana wa Yerohamu, mwana wa Pashuri, mwana wa Malkiya, Maasai, mwana wa Adieli, mwana wa Yahzera, mwana wa Meshulamu, mwana wa Meshilemithi, mwana wa Imeri. 13 Makuhani waliokuwa viongozi wa jamaa zao walikuwa 1,760. Walikuwa watu wenye uwezo, waliowajibika kuhudumu katika nyumba ya Mungu. Jamaa Za Walawi 14 
 • Jamaa za Walawi walikuwa:
 • Shemaya, mwana wa Hashubu, mwana wa Azrikamu, mwana wa Hashabia, wa wana wa Merari.
15 Bakbakari, Hereshi, Galali na Matania mwana wa Mika, mwana wa Zikri, mwana wa Asafu. 16 Obadia mwana wa Shemaya, mwana wa Galali, mwana wa Yeduthuni. Berekia mwana wa Asa, mwana wa Elikana, ambao waliishi katika vijiji vya Wanetofathi. Jamaa Za Mabawabu 17 
 • Mabawabu katika Hekalu la BWANA waliorudi walikuwa:
 • Shalumu, Akubu, Talmoni, Ahimani na ndugu zao. Shalumu alikuwa mlinzi wao mkuu.
18 Walikuwa wamewekwa katika lango la mfalme lililokuwa upande wa mashariki, mpaka wakati huu. Hawa walikuwa mabawabu wa kutoka kwenye kambi ya Walawi. 19 Shalumu mwana wa Kore, mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora, pamoja na mabawabu wenzake kutoka jamaa yake (ya Wakora) waliwajibika kulinda sakafu ya kupuria nafaka ya Hema, kama vile baba zao walivyokuwa wamewajibika kulinda ingilio la Maskani. 20 Hapo zamani Finehasi mwana wa Eleazari alikuwa kiongozi wa mabawabu, naye BWANA alikuwa pamoja naye: 21 Zekaria mwana wa Meshelemia alikuwa bawabu katika ingilio la Hema la Kukutania. 22 Jumla ya waliochaguliwa kuwa mabawabu katika sakafu za kupuria nafaka walikuwa watu 212. Waliandikishwa kwa koo zao kwenye vijiji vyao. Mabawabu hawa waliwekwa katika nafasi zao walizokabidhiwa na Mfalme Daudi pamoja na mwonaji Samweli. 23 Wao na wazao wao walikuwa viongozi wa kulinda malango ya nyumba ya BWANA, nyumba iliyoitwa Hema. 24 Mabawabu walikuwa pande zote nne: mashariki, magharibi, kaskazini na kusini. 25 Ndugu zao katika vijiji vyao walikuwa wakija mara kwa mara na kuwasaidia katika kazi zao kwa vipindi mbalimbali vya siku saba. 26 Lakini mabawabu wanne wakuu, ambao walikuwa Walawi, walikabidhiwa wajibu kwa ajili ya vyumba na hazina katika nyumba ya Mungu. 27 Walikesha mahali walipowekwa kuizunguka nyumba ya Mungu, kwa sababu iliwapasa kuilinda. Pia walitunza funguo kwa ajili ya kufungua mlango kila siku asubuhi.

28 Baadhi yao walikuwa viongozi wa kutunza vifaa vilivyotumika katika huduma ndani ya Hekalu, walivihesabu kila vilipoingizwa ndani na kila vilipotolewa. 29 Wengine walipangiwa kutunza mapambo na vifaa vingine vya patakatifu, pamoja na unga, divai, mafuta, uvumba na vikolezo. 30 Lakini baadhi ya makuhani walifanya kazi ya kuchanganya vikolezo. 31 Mlawi aliyeitwa Metithia, mwana mzaliwa wa kwanza wa Shalumu, wa ukoo wa Kora, alikabidhiwa wajibu kwa ajili ya kuoka mikate ya sadaka. 32 Baadhi ya ndugu zao wa ukoo wa Kohathi walikuwa viongozi wa kuandaa mikate Mitakatifu kwa ajili ya kila Sabato, mikate iliyokuwa inawekwa mezani.

33 Wale waliokuwa waimbaji, viongozi wa jamaa za Walawi, waliishi katika vyumba vya Hekalu, nao hawakufanya shughuli nyingine yo yote kwa sababu iliwapasa kuwajibika kwa kazi hiyo mchana na usiku.

34 Hawa wote walikuwa viongozi wa jamaa za Walawi, wakuu kama walivyoorodheshwa katika koo zao, nao waliishi Yerusalemu.

Ukoo Wa Sauli

35 
 • Baba yake Yaieli aliishi huko Gibeoni.
 • Mkewe aliitwa Maaka,
36 mwanawe mzaliwa wa kwanza aliitwa Abdoni, akafuatiwa na Zuri, Kishi, Baali, Neri, Nadabu, 37 Gedori, Ahio, Zekaria na Miklothi. 38 Miklothi akamzaa Shimeamu. Wao pia waliishi karibu na jamaa zao huko Yerusalemu. 39 Neri akamzaa Kishi, Kishi akamzaa Sauli. Sauli akawazaa Yonathani, Malki-Shua, Abinadabu na Esh-Baali 9.39 Anajulikana pia kwa jina la Ish-Boshethi, maana yake Mtu wa Aibu (2 Sam 2:8) . 40 Yonathani akamzaa Merib-Baali 9.40 Pia anajulikana kwa jina la Mefiboshethi , Merib-Baali akamzaa Mika. 41 Wana wa Mika walikuwa: Pithoni, Meleki, Tarea, na Ahazi. 42 Ahazi akamzaa Yara, Yara akawazaa Alemethi, Azmawethi na Zimri, naye Zimri akamzaa Mosa. 43 Mosa akamzaa Binea, Binea akamzaa Refaya, Refaya akamzaa Eleasa, naye Eleasa akamzaa Aseli. 44 Aseli alikuwa na wana sita, na haya ndiyo majina yao: Azrikamu, Bokeru, Ishmaeli, Shearia, Obadia na Hanani. Hawa ndio waliokuwa wana wa Aseli.
Copyright information for Neno