Ecclesiastes 7

Hekima

1 aAfadhali sifa nzuri kuliko manukato safi,
nayo siku ya kufa kuliko ya kuzaliwa.
2 bAfadhali kwenda kwenye nyumba ya msiba
kuliko kwenda kwenye nyumba ya karamu,
kwa kuwa kifo ni hatima ya kila mwanadamu,
imewapasa walio hai kuliweka hili mioyoni mwao.
3 cHuzuni ni afadhali kuliko kicheko,
kwa sababu uso wenye huzuni wafaa kwa moyo.
4 dMoyo wa wenye hekima uko katika nyumba ya msiba,
lakini moyo wa wapumbavu uko katika nyumba ya anasa.
5 eAfadhali kusikia karipio la mtu mwenye hekima,
kuliko kusikiliza wimbo wa wapumbavu.
6 fKama ilivyo kuvunjika kwa miiba chini ya sufuria,
ndivyo kilivyo kicheko cha wapumbavu.
Hili nalo pia ni ubatili.

7 gDhuluma humfanya mtu mwenye hekima kuwa mpumbavu,
nayo rushwa huuharibu moyo.

8 hMwisho wa jambo ni bora kuliko mwanzo wake,
uvumilivu ni bora kuliko kiburi.
9 iUsiwe mwepesi kukasirika rohoni mwako,
kwa kuwa hasira hukaa kifuani mwa wapumbavu.

10Usiseme, “Kwa nini siku za kale zilikuwa bora kuliko siku hizi?”
Kwa maana si hekima kuuliza maswali kama hayo.

11 jHekima, kama ulivyo urithi, ni kitu chema
na huwafaidia wale walionalo jua.
12Hekima ni ulinzi kama fedha ilivyo ulinzi,
lakini faida ya maarifa ni hii:
kwamba hekima huhifadhi maisha ya aliye nayo.
13 kTafakari kile Mungu alichokitenda:

Nani awezaye kunyoosha
kile ambacho yeye amekipinda?
14 lNyakati zikiwa nzuri, ufurahi,
lakini nyakati zikiwa mbaya, tafakari:
Mungu amefanya hiyo moja,
naam, sanjari
Sanjari hapa maana yake mwandamano wa vitu, wanyama au watu.
na hiyo nyingine.
Kwa hiyo, mwanadamu hawezi kugundua
kitu chochote kuhusu maisha yake ya baadaye.
15 nKatika maisha haya yangu ya ubatili nimeshaona haya mawili:

mtu mwadilifu akiangamia katika uadilifu wake,
naye mtu mwovu akiishi maisha marefu katika uovu wake.
16Usiwe mwenye haki kupita kiasi,
wala usiwe na hekima kupita kiasi:
kwa nini kujiangamiza mwenyewe?
17 oUsiwe mwovu kupita kiasi,
wala usiwe mpumbavu:
kwa nini kufa kabla ya wakati wako?
18 pNi vyema kushika hilo moja
na wala usiache hilo jingine likupite.
Mtu amchaye Mungu ataepuka huko kupita kiasi.
Au: atafuata hayo yote mawili.


19 rHekima humfanya yeye aliye nayo kuwa na uwezo zaidi
kuliko watawala kumi katika mji.

20 sHakuna mtu mwenye haki duniani
ambaye hufanya mambo ya haki
na kamwe asitende dhambi.

21 tUsitie maanani kila neno linalosemwa na watu,
la sivyo, waweza kumsikia
mtumishi wako akikulaani:
22kwa kuwa unafahamu moyoni mwako
kwamba wewe mwenyewe mara nyingi
umewalaani wengine.
23 uYote haya niliyajaribu kwa hekima, nikasema,

“Nimeamua kuwa na hekima”:
lakini hii ilikuwa nje ya uwezo wangu.
24 vVyovyote hekima ilivyo,
hekima iko mbali sana na imejificha,
ni nani awezaye kuigundua?
25 wNikageuza fikira zangu ili kuelewa,
kuchunguza na kuitafuta hekima
na kusudi la mambo,
na ili kuelewa ujinga wa uovu,
na wazimu wa upumbavu.

26 xNimeona jambo lililo chungu kuliko mauti,
mwanamke ambaye ni mtego,
ambaye moyo wake ni wavu wa kutegea
na mikono yake ni minyororo.
Mtu ampendezaye Mungu atamkwepa,
bali mwenye dhambi atanaswa naye.
27Mhubiri anasema, “Tazama, hili ndilo nililogundua:

“Nimegundua kitu kimoja baada ya kingine nilipokuwa katika kusudi la mambo:
28 yningali natafiti
lakini sipati:
nilimpata mwanaume mmoja mnyofu miongoni mwa elfu,
lakini hakuna mwanamke mmoja mnyofu miongoni mwao.
29Hili ndilo peke yake nililolipata:
Mungu amemuumba mwanadamu mnyofu,
lakini mwanadamu amebuni mambo mengi.”
Copyright information for SwhNEN