Hosea 6

Israeli Asiye Na Toba

“Njoni, tumrudie BWANA.
Ameturarua vipande vipande
lakini atatuponya;
ametujeruhi lakini
atatufunga majeraha yetu.
Baada ya siku mbili atatufufua;
katika siku ya tatu atatuinua,
ili tuweze kuishi mbele zake.
Tumkubali BWANA,
tukaze kumkubali yeye.
Kutokea kwake ni hakika kama vile
kuchomoza kwa jua;
atatujia kama mvua za masika,
kama vile mvua za vuli
ziinyweshavyo nchi.”
“Nifanye nini nawe, Efraimu?
Nifanye nini nawe, Yuda?
Upendo wako ni kama ukungu wa asubuhi,
kama umande wa alfajiri utowekao.
Kwa hiyo ninawakata ninyi vipande vipande
kwa kutumia manabii wangu;
nimewaua ninyi kwa maneno ya kinywa changu,
hukumu zangu zinawaka
kama umeme juu yenu.
Kwa maana nataka rehema, wala si dhabihu,
kumkubali Mungu zaidi
kuliko sadaka za kuteketezwa.
Wamevunja Agano kama Adamu:
huko hawakuwa waaminifu kwangu.
Gileadi ni mji wenye watu waovu,
umetiwa madoa kwa nyayo za damu.
Kama wanyang'anyi wamviziavyo mtu,
ndivyo magenge ya makuhani wafanyavyo;
wanaulia watu kwenye njia iendayo Shekemu,
wakifanya uhalifu wa aibu.
10 Nimeona jambo la kutisha
katika nyumba ya Israeli.
Huko Efraimu amejitolea kwa ukahaba
na Israeli amenajisika.
11 “Pia kwa ajili yako, Yuda,
mavuno yameamuriwa.
“Wakati wo wote ningerejesha neema ya watu wangu,
Copyright information for Neno