Job 25

Bildadi Anasema: Mwanadamu Awezaje Kuwa Mwadilifu Mbele Za Mungu?

1 aNdipo Bildadi Mshuhi akajibu:

2 b“Mamlaka na kuheshimiwa ni vyake Mungu;
yeye huthibitisha amani katika mbingu juu.
3 cJe, majeshi yake yaweza kuhesabika?
Ni nani asiyeangaziwa na nuru yake?
4 dMtu awezaje kuwa mwadilifu mbele za Mungu?
Awezaje mtu aliyezaliwa na mwanamke kuwa safi?
5 eIkiwa hata mwezi sio mwangavu
nazo nyota si safi machoni pake,
6 fsembuse mtu ambaye ni funza:
mwanadamu ambaye ni buu tu!”
Copyright information for SwhNEN