Joshua 13

Sehemu Za Kanaani Ambazo Hazijatwaliwa

Yoshua alipokuwa mzee na umri wake ukiwa umesogea sana, BWANA akamwambia, “Wewe ni mzee sana, na bado kumesalia sehemu kubwa sana za nchi ambazo ni za kutwaliwa.

“Haya ndiyo maeneo ambayo bado hayajatekwa: maeneo yote ya Wafilisti na Wageshuri: Eneo hili linaanzia Mto Shihori ulioko mashariki mwa Misri, kuelekea kaskazini kwenye mpaka wa Ekroni, ambayo yote ilihesabiwa kuwa ya Wakanaani (ambako kuna miji mitano ya watawala wa Kifilisti, ambayo ni Gaza, Ashdodi, Ashkeloni, Gathi na Ekroni: ndiyo nchi ya Waavi); kuanzia upande wa kusini, eneo lote la Wakanaani, kuanzia Ara ambayo ni ya Wasidoni, ikienea hadi Afeki, na nchi ya Waamori, eneo la Wagebali
13:5 Yaani eneo la Bubilo, mji wa zamani sana wa Ufoinike (kama kilomita 80 kaskazini mwa Beiruti)
; na sehemu yote ya Lebanoni kuelekea mashariki, kuanzia Baal-Gadi chini ya Mlima Hermoni hadi Lebo-Hamathi.

“Nayo nchi yote ya vilima kuanzia Lebanoni hadi Misrefoth-Maimu, pamoja na eneo lote la Wasidoni, mimi mwenyewe nitawafukuza watoke mbele ya Waisraeli, hakikisha umeligawa eneo hili kwa Israeli kuwa urithi, kama nilivyokuamuru, sasa basi, ligawanye eneo hili kwa yale makabila tisa na ile nusu ya kabila la Manase kuwa urithi.”

Mgawanyo Wa Nchi Mashariki Ya Yordani

Ile nusu nyingine ya kabila la Manase, Wareubeni na Wagadi, wao walishapokea urithi Mose aliokuwa amewapa mashariki ya Yordani, sawasawa na mtumishi wa BWANA alivyowagawia.

Eneo lao lilienea toka Aroeri, iliyoko ukingoni mwa Bonde la Arnoni kuanzia mji ulio katikati ya bonde, ikijumuisha nchi ya uwanda wa juu wote wa Medeba mpaka Diboni, 10 nayo miji yote ya Sihoni mfalme wa Waamori, aliyetawala Heshboni, hadi mpakani mwa Waamori. 11 Vile vile ilijumuisha Gileadi, nchi ya Wageshuri na Wamaaka, mlima wote wa Hermoni na Bashani yote hadi Saleka, 12 yaani ufalme wote wa Ogu katika Bashani, waliokuwa wametawala katika Ashtarothi na Edrei ambao ndio mabaki ya Warefai. Mose alikuwa amewashinda na kuteka nchi yao. 13 Lakini Waisraeli hawakuwafukuza watu wa Geshuri na wa Maaka, kwa hiyo wanaendelea kuishi miongoni mwa Waisraeli mpaka leo hii.14 Lakini kabila la Lawi, Mose hakuwapa urithi, kwa kuwa sadaka za kuteketezwa kwa moto zilizotolewa kwa BWANA, Mungu wa Israeli, ndizo zilizokuwa urithi wao, kama alivyowaahidi.15 Haya ndiyo maeneo ambayo Mose alikuwa amewapa kabila la Reubeni ukoo kwa ukoo:

16 Kuanzia nchi ya Aroeri iliyo ukingoni mwa Bonde la Aroni, na kuanzia mji ulio katikati ya bonde, pia uwanda wote wa juu kupita Madeba 17 mpaka Heshboni na miji yake yote kwenye uwanda wa juu, ikiwa ni pamoja na Diboni, Bamoth-Baali, Beth-Baal-Meoni, 18 Yahasa, Kedemothi, Mefaathi, 19 Kiriathaimu, Sibma, Sereth-Shahari juu ya kilima kilicho katika bonde, 20 Beth-Peori, matelemko ya Pisga na Beth-Yeshimothi: 21 miji yote ya uwanda wa juu na eneo lote la utawala wa Sihoni mfalme wa Waamori, aliyetawala Heshboni. Mose alikuwa amemshinda Sihoni, pia watawala wakuu wa Wamidiani, ambao ni Evi, Rekemu, Suri, Huri na Reba, waliokuwa wameungana na Sihoni, ambao waliishi katika nchi ile. 22 Pamoja na wale waliouawa katika vita, Waisraeli walikuwa wamemwua kwa upanga Balaamu mwana wa Beori aliyekuwa nabii. 23 Mpaka wa Wareubeni ulikuwa ni ukingo wa Mto Yordani. Miji hii ndiyo iliyokuwa urithi wa Wareubeni ukoo kwa ukoo.24 Haya ndiyo maeneo ambayo Mose alikuwa amewagawia kabila la Gadi, ukoo kwa ukoo:

25 Nchi ya Yazeri, miji yote ya Gileadi na nusu ya nchi ya Amoni mpaka Aroeri, karibu na Raba; 26 kuanzia Heshboni mpaka Ramath-Mizpa na Betonimu, tena kutoka Mahanaimu hadi nchi ya Debiri; 27 tena katika bonde, Beth-Haramu, Beth-Nimra, Sukothi na Safoni na sehemu iliyobaki ya eneo la utawala wa Sihoni mfalme wa Heshboni (upande wa mashariki wa Mto Yordani, nchi inayoishia kwenye Bahari ya Kinerethi
13:27 Yaani Bahari ya Galilaya
).
28 Miji hii na vijiji vyake vilikuwa urithi wa kabila la Gadi ukoo kwa ukoo.29 Haya ndiyo maeneo ambayo Mose alikuwa amewapa hiyo nusu ya kabila la Manase, yaani kwa nusu ya jamaa ya uzao wa Manase, ukoo kwa ukoo:

30 Nchi iliyoenea kuanzia Mahanaimu, pamoja na Bashani yote, ufalme wote wa Ogu mfalme wa Bashani, makazi yote ya Yairi huko Bashani, miji sitini, 31 nusu ya Gileadi, Ashtarothi na Edrei (miji ya kifalme ya Ogu katika Bashani). Hii ilikuwa kwa ajili ya wazao wa Makiri mwana wa Manase, kwa ajili ya nusu ya wana wa Makiri, ukoo kwa ukoo.32 Huu ndio urithi alioutoa Mose wakati alipokuwa katika tambarare za Moabu, ng'ambo ya Yordani mashariki ya Yeriko. 33 Lakini kwa kabila la Walawi, Mose hakuwapa urithi; BWANA Mungu, Mungu wa Israeli ndiye urithi wao, kama alivyowaahidi.

Copyright information for Neno