Nehemiah 7

1Baada ya ukuta kukamilika kujengwa upya na kuweka milango, waliteuliwa mabawabu wa lango, waimbaji na Walawi. 2Nikamweka Hanani ndugu yangu kuwa kiongozi wa Yerusalemu, pamoja na Hanania jemadari wa ngome, kwa kuwa alikuwa mtu mwadilifu na mwenye kumcha Mungu kuliko watu wengine. 3Nikawaambia, “Malango ya Yerusalemu yasifunguliwe mpaka jua litakapokuwa limepanda. Wakati walinzi wa malango wakiwa kwenye zamu, wafunge milango na waweke makomeo. Pia wateueni wenyeji wa Yerusalemu wawe walinzi, kila mmoja kwenye lindo lake na wengine karibu na nyumba zao wenyewe.”

Orodha Ya Waliorudi Toka Uhamishoni

4Mji ulikuwa mkubwa tena wenye nafasi nyingi, lakini walikuwepo watu wachache ndani yake, nazo nyumba zilikuwa bado ni magofu. 5Hivyo Mungu wangu akaweka moyoni mwangu kuwakusanya wakuu, maafisa na watu wa kawaida kwa ajili ya kuorodheshwa kulingana na jamaa zao. Nilikuta orodha ya vizazi iliyoandikwa ya wale waliokuwa wa kwanza kurudi toka utumwani. Haya ndiyo niliyokuta yameandikwa humo:6Hawa ndio watu wa jimbo waliorudi kutoka utumwani uhamishoni walikokuwa wamepelekwa na Mfalme Nebukadneza wa Babeli (walirudi Yerusalemu na Yuda, kila mmoja kwenye mji wake,
7wakiwa wamefuatana na Zerubabeli, Yeshua, Nehemia, Azaria, Raamia, Nahamani, Mordekai, Bilshani, Mispereti, Bigwai, Nehumu na Baana):Orodha ya watu wa Israeli:

8wazao wa Paroshi 2,172 9wazao wa Shefatia 372 10wazao wa Ara 652 11wazao wa Pahath-Moabu (kupitia ukoo wa Yeshua na Yoabu) 2,818 12wazao wa Elamu 1,254 13wazao wa Zatu 845 14wazao wa Zakai 760 15wazao wa Binui 648 16wazao wa Bebai 628 17wazao wa Azgadi 2,322 18wazao wa Adonikamu 667 19wazao wa Bigwai 2,067 20wazao wa Adini 655 21wazao wa Ateri (kupitia Hezekia) 98 22wazao wa Hashumu 328 23wazao wa Besai 324 24wazao wa Harifu 112 25wazao wa Gibeoni 95 27watu wa Anathothi 128 28watu wa Beth-Azmawethi 42 29watu wa Kiriath-Yearimu, Kefira na Beerothi 743 30watu wa Rama na Geba 621 31watu wa Mikmashi 122 32watu wa Betheli na Ai 123 33watu wa Nebo 52 34watu wa Elamu 1,254 35watu wa Harimu 320 36watu wa Yeriko 345 37watu wa Lodi, Hadidi na Ono 721 38watu wa Senaa 3,930
39

Makuhani:

40wazao wa Imeri 1,052 41wazao wa Pashuri 1,247 42wazao wa Harimu 1,017
43

Walawi:

44

Waimbaji:

45

  • Mabawabu wa malango:

46Wanethini
7.46 Yaani watumishi wa Hekalu (pia 7:46, 60, 73)
wa Hekaluni:
  • wazao wa
  • Siha, Hasufa, Tabaothi,
47Kerosi, Sia, Padoni, 48Lebana, Hagaba, Shalmai, 49Hanani, Gideli, Gahari, 50Reaya, Resini, Nekoda, 51Gazamu, Uza, Pasea, 52Besai, Meunimu, Nefusimu, 53Bakbuki, Hakufa, Harhuri, 54Basluthi, Mehida, Harsha, 55Barkosi, Sisera, Tema, 56Nesia na Hatifa. 57Wazao wa watumishi wa Solomoni:
  • wazao wa
  • Sotai, Soferethi, Perida,
58Yaala, Darkoni, Gideli, 59Shefatia, Hatili, Pokereth-Hazebaimu na Amoni. 60Wanethini wote na wazao wa watumishi wa Solomoni 392
61

Wafuatao ni watu waliorudi kutoka miji ya Tel-Mela, Tel-Harsha, Kerubu, Adoni na Imeri, lakini hawakuweza kuthibitisha kwamba jamii zao zilitokana na Israeli:

62wazao wa Delaya, Tobia na Nekoda 642 63

Na kutoka miongoni mwa makuhani:
  • wazao wa
  • Hobaya, Hakosi na Barzilai (mtu aliyekuwa amemwoa binti wa Barzilai, Mgileadi, naye akaitwa kwa jina hilo.)


64Hawa walitafuta katika orodha ya jamii zao, lakini hawakuonekana kwa hiyo waliondolewa katika ukuhani kama watu najisi. 65Kwa hiyo, Tirshatha
7.65 Tirshatha ni jina la heshima aliloitwa mtawala wa Yuda chini ya Ufalme wa Uajemi
aliagiza kuwa wasile cho chote miongoni mwa vyakula vitakatifu mpaka atakapopatikana kuhani ahudumuye kwa Urimu na Thumimu
7:65 Urimu na Thumimu maana yake ni Nuru na Kweli; vifaa hivi viliwekwa kwenye kifuko cha juu cha kisibau cha Kuhani Mkuu ili kujua mapenzi ya Mungu kwenye mambo ya kutatanisha
.66Jumla ya watu wote waliorudi kutoka utumwani uhamishoni walikuwa 42,360; 67tena zaidi ya hao walikuwepo watumishi wa kiume na wa kike 7,337; pia walikuwemo waimbaji wanaume na wanawake 245. 68Walikuwako farasi 736, nyumbu 245 69ngamia 435 na punda 6,720.70Baadhi ya wakuu wa mbari walichangia kazi ya ujenzi. Tirshatha alikabidhi kwenye hazina darkoni 1,000
7.70 Darkoni 1,000 za dhahabu ni sawa na uzito wa kilo 8.6
za dhahabu, mabakuli 50 na mavazi 530 kwa ajili ya makuhani.
71Baadhi ya wakuu wa mbari walikabidhi kwenye hazina kwa ajili ya kazi darkoni 20,000 za dhahabu
7.71 Darkoni 20,000 za dhahabu ni sawa na kilo 172
na mane 2,200
7.71 Mane 2,200 za fedha ni sawa na kilo 1,300
za fedha.

72Jumla ya matoleo ya watu wengine yalikuwa ni darkoni 20,000 za dhahabu, mane 2,000 za fedha na mavazi sitini na saba ya makuhani.

73Makuhani, Walawi, mabawabu wa malango, waimbaji na Wanethini, pamoja na baadhi ya watu wengine na Waisraeli wengine wote, waliishi katika miji yao wenyewe.

Ezara Asoma Sheria

Ilipotimia miezi saba, nao Waisraeli wakiwa tayari wanaishi katika miji yao,

Copyright information for Neno