Psalms 131

Maombi Ya Kumtegemea Mungu Kwa Unyenyekevu

(Wimbo Wa Kwenda Juu. Wa Daudi.)

Moyo wangu hauna kiburi, Ee BWANA,
macho yangu hayajivuni;
sijishughulishi na mambo makuu kunizidi
wala mambo ya ajabu mno kwangu.
Lakini nimetuliza na kunyamazisha nafsi yangu;
kama mtoto aliyeachishwa kunyonya na mama yake,
kama mtoto aliyeachishwa kunyonya
ndivyo ilivyo nafsi iliyoko ndani yangu.
Ee Israeli, mtumaini BWANA
tangu sasa na hata milele.
Copyright information for Neno