Psalms 134

Wito Wa Kumsifu Mungu

(Wimbo Wa Kwenda Juu)

Msifuni BWANA, ninyi nyote
watumishi wa BWANA,
ninyi mnaotumika usiku
ndani ya nyumba ya BWANA.
Inueni mikono yenu katika mahali patakatifu
na mumsifu BWANA.
Naye BWANA, Muumba wa mbingu na dunia,
awabariki kutoka Sayuni.
Copyright information for Neno