Psalms 14

Uovu Wa Wanadamu

(Kwa Mwimbishaji: Mtindo Wa Mahalathi. Zaburi Ya Daudi)

1Mpumbavu anasema moyoni mwake,
“Hakuna Mungu.”
Wameharibika, matendo yao ni maovu kabisa;
hakuna atendaye mema.
2Toka mbinguni BWANA anawachungulia
wanadamu chini
aone kama wako wenye akili,
wo wote wanaomtafuta Mungu.
3Wote wamepotoka,
wameoza wote pamoja;
hakuna atendaye mema,
naam! Hata mmoja.
4Je, watendao mabaya hawatajifunza:
wale ambao huwala watu wangu
kama watu walavyo mkate,
hao ambao hawamwiti BWANA?
5Hapo ndipo walipo, wameingiwa na hofu nyingi,
maana Mungu yupo pamoja na wenye haki.
6Ninyi watenda mabaya mnakwamisha mipango ya maskini,
bali BWANA ni kimbilio lao.
7Laiti wokovu wa Israeli
ungalikuja kutoka Sayuni!
Wakati BWANA arejeshapo
wafungwa wa watu wake,
Yakobo na ashangilie,
Israeli na afurahi!
Copyright information for Neno