Psalms 149

Wimbo Wa Kumsifu Mungu Kwa Wema Wake

Msifuni BWANA.
Mwimbieni BWANA wimbo mpya,
sifa zake katika kusanyiko la watakatifu.
Israeli na washangilie katika Muumba wao,
watu wa Sayuni na wafurahi katika mfalme wao.
Na walisifu jina lake kwa kucheza
na wampigie muziki kwa matari na kinubi.
Kwa maana BWANA anapendezwa na watu wake,
anawavika wanyenyekevu taji ya wokovu.
Watakatifu na washangilie katika heshima hii
na waimbe kwa shangwe vitandani mwao.
Sifa za Mungu na ziwe vinywani mwao
na upanga ukatao kuwili mikononi mwao,
ili walipize mataifa kisasi
na adhabu juu ya mataifa,
wawafunge wafalme wao kwa minyororo,
wakuu wao kwa pingu za chuma,
ili kuwafanyia hukumu iliyoandikwa dhidi yao.
Huu ndio utukufu wa watakatifu wake wote.
Msifuni BWANA.
Copyright information for Neno