Psalms 150

Msifuni BWANA Kwa Ukuu Wake

Msifuni BWANA.
Msifuni Mungu katika patakatifu pake,
msifuni katika mbingu zake kuu.
Msifuni kwa matendo yake makuu,
msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake.
Msifuni kwa mvumo wa tarumbeta,
msifuni kwa kinubi na zeze,
Msifuni kwa matari na kucheza,
msifuni kwa kinanda cha nyuzi na filimbi,
Msifuni kwa matoazi yaliayo,
msifuni kwa matoazi yavumayo sana.
Kila chenye pumzi na kimsifu BWANA.
Msifuni BWANA. Haleluya!
Copyright information for Neno