Psalms 3

Sala Ya Asubuhi Ya Kuomba Msaada

(Zaburi Ya Daudi Alipomkimbia Absalomu)

Ee BWANA, tazama adui zangu walivyo wengi!
Ni wengi kiasi gani wanaoinuka dhidi yangu!
Wengi wanasema juu yangu,
“Mungu hatamwokoa.”
Lakini wewe, Ee BWANA, ni ngao pande zote;
umeniwekea utukufu na kuinua kichwa changu.
Ninamlilia BWANA kwa sauti kuu,
naye ananijibu kutoka katika mlima wake mtakatifu.
Ninajilaza na kupata usingizi;
naamka tena, kwa maana BWANA hunitegemeza.
Sitaogopa makumi elfu ya adui,
wanaojipanga dhidi yangu kila upande.
Ee BWANA, amka!
Uniokoe, Ee Mungu wangu!
Wapige adui zangu wote kwenye taya,
vunja meno ya waovu.
Kwa maana wokovu watoka kwa BWANA.
Baraka yako na iwe juu ya watu wako.
Copyright information for Neno