Psalms 41

Maombi Ya Mtu Mgonjwa

(Kwa Mwimbishaji: Zaburi Ya Daudi)

Heri mtu yule anayemjali mnyonge,
BWANA atamwokoa wakati wa shida.
BWANA atamlinda na kuyahifadhi maisha yake,
atambariki katika nchi
na hatamwacha katika tamaa ya adui zake.
BWANA atamtegemeza awapo mgonjwa kitandani,
atamwinua kutoka kitandani mwake.
Nilisema, “Ee BWANA nihurumie,
niponye, maana nimekutenda dhambi wewe.”
Adui zangu wanasema kwa hila,
“Lini atakufa na jina lake litokomee kabisa.”
Kila anapokuja mtu kunitazama,
huzungumza uongo,
huku moyo wake hukusanya masingizio;
kisha huondoka na kuyasambaza huko na huko.
Adui zangu wote hunong'onezana dhidi yangu,
hao huniwazia mabaya sana, wakisema,
“Ugonjwa mbaya sana umempata,
kamwe hatainuka tena kitandani mwake.”
Hata rafiki yangu wa karibu, niliyemwamini,
yule aliyekula chakula changu
ameniinulia kisigino chake.
10 Lakini wewe, Ee BWANA, unihurumie,
ukaniinue tena, ili niweze kuwalipiza kisasi.
11 Najua kwamba wapendezwa nami,
kwa kuwa adui yangu hanishindi.
12 Katika uadilifu wangu unanitegemeza
na kuniweka kwenye uwepo wako milele.
13 Msifuni BWANA, Mungu wa Israeli,
tangu milele na hata milele.
Amen na Amen.

Copyright information for Neno