Psalms 49

Upumbavu Wa Kutegemea Mali

Kwa mwimbishaji. Zaburi ya wana wa Kora.

1 aSikieni haya, enyi mataifa yote,
sikilizeni, ninyi wote mkaao dunia hii.
2 bWakubwa kwa wadogo,
matajiri na maskini pamoja:
3 cKinywa changu kitasema maneno ya hekima,
usemi wa moyo wangu utatoa ufahamu.
4 dNitatega sikio langu nisikilize mithali,
nitafafanua kitendawili kwa zeze:

5 eKwa nini niogope siku mbaya zinapokuja,
wakati wadanganyifu waovu wanaponizunguka,
6 fwale wanaotegemea mali zao
na kujivunia utajiri wao mwingi?
7 gHakuna mwanadamu awaye yote
awezaye kuukomboa uhai wa mwingine,
au kumpa Mungu fidia kwa ajili yake.
8 hFidia ya uhai ni gharama kubwa,
hakuna malipo yoyote yanayotosha,
9 iili kwamba aishi milele
na asione uharibifu.

10 jWote wanaona kwamba watu wenye hekima hufa;
wajinga na wapumbavu vivyo hivyo huangamia
na kuwaachia wengine mali zao.
11 kMakaburi yao yatabaki kuwa nyumba zao za milele,
makao yao vizazi vyote;
ingawa walikuwa na mashamba
na kuyaita kwa majina yao.

12 lLakini mwanadamu, licha ya utajiri wake, hadumu;
anafanana na mnyama aangamiaye.

13 mHii ndiyo hatima ya wale wanaojitumainia wenyewe,
pia ya wafuasi wao, waliothibitisha misemo yao.
14 nKama kondoo, wamewekewa kwenda kaburini,
Kaburini hapa ina maana ya Sheol kwa Kiebrania, yaani Kuzimu.

nacho kifo kitawala.
Wanyofu watawatawala asubuhi,
maumbile yao yataozea kaburini,
mbali na majumba yao makubwa ya fahari.
15 pLakini Mungu atakomboa uhai
Au: nafsi.
wangu na kaburi,
hakika atanichukua kwake.

16Usitishwe mtu anapotajirika,
fahari ya nyumba yake inapoongezeka,
17 rkwa maana hatachukua chochote atakapokufa,
fahari yake haitashuka pamoja naye.
18 sIngawa alipokuwa akiishi alijihesabu kuwa heri,
na wanadamu wanakusifu unapofanikiwa,
19 tatajiunga na kizazi cha baba zake,
ambao hawataona kamwe nuru ya uzima.

20 uMwanadamu mwenye utajiri bila ufahamu
ni kama wanyama waangamiao.
Copyright information for SwhNEN