Psalms 70

Kuomba Msaada

(Za 40:13-17)

(Kwa Mwimbishaji: Zaburi Ya Daudi. Maombolezo)

Ee Mungu, ufanye haraka kuniokoa,
Ee BWANA, njoo hima unisaidie.
Waaibike na kufedheheshwa
wale wanaotafuta uhai wangu;
wale wanaotamani kuangamizwa kwangu
warudishwe nyuma kwa aibu.
Wale waniambiao, “Aha! Aha!”
warudi nyuma kwa sababu ya aibu yao.
Lakini wote wakutafutao
na washangilie na kukufurahia,
wale wapendao wokovu wako daima na waseme,
“Mungu na atukuzwe!”
Hata sasa mimi ni maskini na mhitaji;
Ee Mungu, unijie haraka.
Wewe ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu;
Ee BWANA, usikawie.
Copyright information for Neno