Psalms 83

Maombi Kwa Ajili Ya Kushindwa Kwa Adui Wa Israeli

(Zaburi Ya Asafu. Wimbo)

1Ee Mungu, usinyamaze kimya,
usinyamaze, Ee Mungu usitulie.
2Tazama watesi wako wanafanya fujo,
jinsi adui zako wanavyoinua vichwa vyao.
3Kwa hila wanafanya shauri dhidi ya watu wako,
wanafanya shauri baya dhidi ya wale unaowapenda.
4Wanasema, “Njoni,
tuwaangamize kama taifa,
ili jina la Israeli lisikumbukwe tena.”
5Kwa nia moja wanapanga pamoja mashauri mabaya,
wanafanya muungano dhidi yako,
6mahema ya Edomu na Waishmaeli,
ya Wamoabu na Wahagari,
7Gebali
83.7 Yaani Bubilo, mji wa zamani sana wa Ufoinike (kama kilomita 80 kaskazini mwa Beiruti)
, Amoni na Ameleki,
Ufilisti, pamoja na watu wa Tiro.
8Pia Ashuru wameungana nao
kuwapa nguvu wazao wa Loti.
9Uwatendee kama vile ulivyowatendea Midiani,
na kama vile ulivyowatendea Sisera na Yabini
penye kijito cha Kishoni,
10ambao waliangamia huko Endori
na wakawa kama takataka juu ya nchi.
11Wafanye wakuu wao kama Orebu na Zebu,
watawala wao kama Zeba na Zalmuna,
12ambao walisema, “Na tumiliki nchi
ya malisho ya Mungu.”
13Ee Mungu wangu, wapeperushe
kama mavumbi ya kisulisuli,
kama makapi yapeperushwayo na upepo.
14Kama vile moto uteketezavyo msitu
au mwali wa moto unavyounguza milima,
15kwa hiyo wafuatilie kwa tufani yako
na kuwafadhaisha kwa dhoruba yako.
16Funika nyuso zao kwa aibu
ili watu walitafute jina lako, Ee BWANA.
17Wao na waaibishwe na kufadhaishwa,
wao na waangamie kwa aibu.
18Na wajue kwamba wewe,
ambaye jina lako ni BWANA,
kwamba wewe peke yako
ndiwe Uliye Juu Sana ya dunia yote.
Copyright information for Neno