Psalms 87

Sifa Za Yerusalemu

(Zaburi. Wimbo Wa Wana Wa Kora)

Ameuweka msingi wake katika mlima mtakatifu;
BWANA anayapenda malango ya Sayuni
kuliko makao yote ya Yakobo.
Mambo matukufu yanasemwa juu yako,
Ee mji wa Mungu:
“Nitaweka kumbukumbu ya Rahabu
87.4 Rahabu hapa ni jina la ushairi la Misri
na Babeli
miongoni mwa wale wanaonikubali mimi:
Ufilisti pia na Tiro, pamoja na Kushi
87.4 Kushi hapa ina maana ya Nile ya juu, yaani Ethiopia
,
nami nitasema, ‘Huyu alizaliwa Sayuni.’ ”
Kuhusu Sayuni itasemwa hivi,
“Huyu na yule walizaliwa humo,
naye Aliye Juu Sana mwenyewe
atamwimarisha.”
BWANA ataandika katika orodha mataifa:
“Huyu alizaliwa Sayuni.
87.6 Au: Mungu atawaorodhesha katika ordha yake ya kifalme kama wenyeji wa mji wake

Watakapokuwa wanapiga vinanda wataimba,
“Chemchemi zangu zote ziko kwako.”
Copyright information for Neno