Psalms 91

Mungu Mlinzi Wetu

1 aYeye akaaye mahali pa salama pake Yeye Aliye Juu Sana,
atadumu katika uvuli wake Mwenyezi.
Mwenyezi hapa ina maana ya Shaddai kwa Kiebrania.

2 cNitasema kumhusu Bwana, “Yeye ndiye kimbilio langu na ngome yangu,
Mungu wangu, ambaye ninamtumaini.”

3 dHakika yeye ataniokoa na mtego wa mwindaji,
na maradhi ya kuambukiza ya kuua.
4 eAtakufunika kwa manyoya yake,
chini ya mbawa zake utapata kimbilio,
uaminifu wake utakuwa ngao na kinga yako.
5 fHutaogopa vitisho vya usiku,
wala mshale urukao mchana,
6wala maradhi ya kuambukiza
yanayonyemelea gizani,
wala tauni iharibuyo adhuhuri.
7Ijapo watu elfu wataangukia kando yako,
kumi elfu mkono wako wa kuume,
lakini haitakukaribia wewe.
8 gUtatazama tu kwa macho yako
na kuona adhabu ya waovu.

9Kama ukimfanya Aliye Juu Sana kuwa makao yako:
naam, Bwana ambaye ni kimbilio langu,
10 hbasi hakuna madhara yatakayokupata wewe,
hakuna maafa yataikaribia hema yako.
11 iKwa kuwa atawaagiza malaika zake kwa ajili yako,
wakulinde katika njia zako zote.
12 jMikononi mwao watakuinua,
ili usijikwae mguu wako kwenye jiwe.
13 kUtawakanyaga simba na nyoka wakali,
simba mkubwa na nyoka utawaponda kwa miguu.

14 l Bwana asema, “Kwa kuwa ananipenda, nitamwokoa;
nitamlinda, kwa kuwa analikiri Jina langu.
15 mAtaniita, nami nitamjibu;
nitakuwa pamoja naye katika taabu,
nitamwokoa na kumheshimu.
16 nKwa siku nyingi nitamshibisha
na kumwonyesha wokovu wangu.”
Copyright information for SwhNEN