Ruth 3

Ruthu Na Boazi Kwenye Sakafu Ya Kupuria

Kisha Naomi akamwambia mkwewe, “Binti yangu, je, nisingelikutafutia pumziko ambako utatunzika vyema? Je, Boazi, ambaye umekuwa pamoja na watumishi wake wasichana, si jamaa yetu wa karibu? Usiku wa leo atakuwa anapepeta ngano kwenye sakafu ya kupuria. Basi oga na ukajipake marashi, ujivalie nguo zako nzuri. Kisha uende kwenye sakafu ya kupuria, lakini angalia asijue kwamba upo pale mpaka atakapomaliza kula na kunywa. Atakapokwenda kulala, angalia mahali atakapolala. Kisha uende ufunue miguu yake, ulale. Naye atakuambia utakalofanya.”

Ruthu akajibu, “Lo lote usemalo nitatenda.” Basi akashuka mpaka kwenye sakafu ya kupuria, akafanya kila kitu mama mkwe wake alichomwambia kufanya.

Wakati Boazi alipomaliza kula na kunywa, naye alikuwa amejawa na furaha, alikwenda kulala mwisho wa lundo la nafaka. Ruthu akakaribia kimya kimya, akafunua miguu yake, akalala. Usiku wa manane kitu kilimshtua Boazi, akajigeuza, akagundua yupo mwanamke amelala miguuni pake.

Akauliza, “Wewe ni nani?”

Akajibu, “Ni mimi Ruthu, mjakazi wako. Uitande nguo yako juu yangu, kwa sababu wewe ndiwe jamaa wa karibu wa kukomboa.”

10 Akamwambia, “Binti yangu, ubarikiwe na BWANA. Wema huu wa sasa ni mkuu kushinda hata ule ulioonyesha mwanzoni. Hukuwakimbilia vijana, wakiwa matajiri au maskini. 11 Sasa, binti yangu, usiogope. Nitakufanyia yote uliyoomba. Kwa maana mji wote wa watu wangu wanakujua ya kwamba wewe ni mwanamke mwenye tabia nzuri. 12 Ingawa ni kweli kwamba mimi ndiye jamaa aliye karibu, lakini kuna mtu mwingine wa jamaa aliye karibu zaidi wa kukomboa kuliko mimi. 13 Wewe kaa hapa usiku huu, kisha asubuhi kama akikubali kukomboa, vyema na akomboe. La sivyo kama hayuko tayari, hakika kama BWANA aishivyo nitafanya hivyo. Lala hapa mpaka asubuhi.”

14 Hivyo huyo mwanamke akalala miguuni pake mpaka asubuhi, akaondoka mapema asijaweza mtu kumtambua mwenzake, maana Boazi alisema, “Isijulikane kabisa ya kuwa mwanamke alifika kwenye sakafu ya kupuria.”

15 Pia akamwambia, “Leta shela yako uliyoivaa, uitandaze.” Naye alipoitandaza, akamimina vipimo sita vya shayiri, akamtwika. Kisha Ruthu akarudi zake mjini.

16 Basi Ruthu alipofika kwa mama mkwe wake Naomi, akamwuliza, “Je, binti yangu, ilikuwaje huko?”

Ndipo akamwelezea kila kitu Boazi alichomfanyia.
17 Akaendelea kusema, “Amenipa shayiri vipimo sita
3.17 Vipimo sita vya shayiri ni sawa na kilo 15
akisema, ‘Usiende kwa mama mkwe wako mikono mitupu.’ ”

18 Kisha Naomi akasema, “Subiri binti yangu, mpaka utakapojua kwamba hili jambo limekwendaje. Kwa sababu mtu huyu hatatulia mpaka akamilishe jambo hili leo.”

Copyright information for Neno