Song of Solomon 1

1Wimbo ulio Bora wa Solomoni.

Shairi La Kwanza

Mpendwa
2Unibusu kwa busu la kinywa chako,
kwa maana upendo wako unafurahisha kuliko divai.
3Manukato yako yananukia vizuri,
jina lako ni kama manukato yaliyomiminwa.
Ndiyo sababu wanawali wanakupenda!
4Nichukue twende nawe, na tufanye haraka!
Mfalme na anilete ndani ya vyumba vyake. Marafiki
Tunakushangilia na kukufurahia,
tutasifu upendo wako zaidi kuliko divai. Mpendwa
Tazama ni jinsi gani ilivyo haki wakupende!
5Mimi ni mweusi, lakini napendeza,
Enyi binti za Yerusalemu,
weusi kama mahema ya Kedari,
kama mapazia ya hema la Solomoni.
6Usinikazie macho kwa sababu mimi ni mweusi,
kwa sababu nimefanywa mweusi na jua.
Wana wa mama yangu walinikasirikia
na kunifanya niwe mtunza mashamba ya mizabibu,
shamba langu mwenyewe la mizabibu nimeliacha.
7Niambie, wewe ambaye ninakupenda,
unalisha wapi kundi lako la kondoo
na ni wapi unapowapumzisha kondoo wako adhuhuri.
Kwa nini niwe kama mwanamke aliyefunikwa shela
karibu na makundi ya rafiki zako? Marafiki
8Kama hujui, ewe mwanamke mzuri kuliko wote,
fuata nyayo za kondoo
na kulisha wana-mbuzi wako
karibu na hema za wachungaji. Mpenzi
9Mpenzi wangu, ninakufananisha na farasi jike
aliyefungwa katika mojawapo ya magari ya vita ya Farao.
10Mashavu yako yanapendeza yakiwa na vipuli,
shingo yako ikiwa na mikufu ya vito.
11Tutakufanyia vipuli vya dhahabu,
vyenye kupambwa kwa fedha. Mpendwa
12Wakati mfalme alipokuwa mezani pake,
manukato yangu yasambaza harufu yake nzuri.
13Mpenzi wangu kwangu mimi ni kifuko cha manemane
kati ya matiti yangu.
14Mpenzi wangu kwangu mimi ni kama kishada cha maua ya mhina
yaliyochanua kutoka mashamba ya mizabibu ya En-Gedi. Mpenzi
15Tazama jinsi ulivyo mzuri, mpenzi wangu!
Tazama jinsi ulivyo mzuri!
Macho yako ni kama ya hua. Mpendwa
16Tazama jinsi ulivyo mzuri, mpenzi wangu!
O, tazama ni jinsi gani unavyopendeza!
Na kitanda chetu ni cha majani mabichi mazuri. Mpenzi
17Nguzo za nyumba yetu ni mierezi,
na mapao yetu ni miberoshi.
Copyright information for Neno