Zechariah 9

Hukumu Juu Ya Adui Za Israeli

1Neno:

aNeno la Bwana liko kinyume na nchi ya Hadraki
na Dameski itakuwa mahali pa kupumzika,
kwa kuwa macho ya watu na ya kabila zote
za Israeli yako kwa Bwana,
2 bpia juu ya Hamathi inayopakana nayo,
juu ya Tiro na Sidoni,
ingawa wana ujuzi mwingi sana.
3 cTiro amejijengea ngome imara,
amelundika fedha kama mavumbi
na dhahabu kama taka za mitaani.
4 dLakini Bwana atamwondolea mali zake
na kuuangamiza uwezo wake wa baharini,
naye atateketezwa kwa moto.
5 eAshkeloni ataona hili na kuogopa;
Gaza atagaagaa kwa maumivu makali,
pia Ekroni, kwa sababu
matumaini yake yatanyauka.
Gaza atampoteza mfalme wake
na Ashkeloni ataachwa pweke.
6 fWageni watakalia mji wa Ashdodi,
nami nitakatilia mbali kiburi cha Wafilisti.
7 gNitaondoa damu vinywani mwao,
chakula kile walichokatazwa kati ya meno yao.
Mabaki yao yatakuwa mali ya Mungu wetu,
nao watakuwa viongozi katika Yuda,
naye Ekroni atakuwa kama Wayebusi.
8 hLakini nitailinda nyumba yangu
dhidi ya majeshi ya wanyangʼanyi.
Kamwe mdhalimu hatashambulia watu wangu tena,
kwa maana sasa ninawachunga.

Kuja Kwa Mfalme Wa Sayuni

9 iShangilia sana, ee Binti Sayuni!
Piga kelele, Binti Yerusalemu!
Tazama, Mfalme wako anakuja kwako,
ni mwenye haki, naye ana wokovu,
ni mpole, naye amepanda punda,
mwana-punda, mtoto wa punda.
10 jNitaondoa magari ya vita kutoka Efraimu
na farasi wa vita kutoka Yerusalemu,
nao upinde wa vita utavunjwa.
Atatangaza amani kwa mataifa.
Utawala wake utaenea kutoka bahari hadi bahari,
na kutoka Mto Frati hadi mwisho wa dunia.
11 kKwako wewe, kwa sababu ya damu ya Agano langu nawe,
nitawaacha huru wafungwa wako
watoke kwenye shimo lisilo na maji.
12 lRudieni ngome yenu, enyi wafungwa wa tumaini;
hata sasa ninatangaza kwamba
nitawarejesheeni maradufu.
13 mNitampinda Yuda kama nipindavyo upinde wangu,
nitamfanya Efraimu mshale wangu.
Nitawainua wana wako, ee Sayuni,
dhidi ya wana wako, ee Uyunani,
na kukufanya kama upanga wa shujaa wa vita.

Bwana Atatokea

14Kisha Bwana atawatokea;
mshale wake utamulika
kama umeme wa radi.
Bwana Mwenyezi atapiga tarumbeta,
naye atatembea katika tufani za kusini,
15 nna Bwana Mwenye Nguvu Zote atawalinda.
Wataangamiza na kushinda
kwa mawe ya kutupa kwa kombeo.
Watakunywa na kunguruma kama waliolewa mvinyo;
watajaa kama bakuli linalotumika kunyunyizia
kwenye pembe za madhabahu.
16 o Bwana Mungu wao atawaokoa siku hiyo
kama kundi la watu wake.
Watangʼara katika nchi yake
kama vito vya thamani kwenye taji.
17Jinsi gani watavutia na kuwa wazuri!
Nafaka itawastawisha vijana wanaume,
nayo divai mpya vijana wanawake.
Copyright information for SwhNEN