1 Timothy 2

Maagizo Kuhusu Kuabudu

1 aAwali ya yote, nasihi kwamba dua, sala, maombezi na shukrani zifanyike kwa ajili ya watu wote: 2 bkwa ajili ya wafalme na wale wote wenye mamlaka, ili tupate kuishi kwa amani na utulivu, katika uchaji wote wa Mungu na utakatifu. 3 cJambo hili ni jema, tena linapendeza machoni pa Mungu Mwokozi wetu, 4 danayetaka watu wote waokolewe na wafikie kuijua kweli. 5 eKwa maana kuna Mungu mmoja na mpatanishi mmoja kati ya Mungu na wanadamu, yaani mwanadamu Kristo Yesu, 6 faliyejitoa mwenyewe kuwa fidia kwa ajili ya wanadamu wote: jambo hili lilishuhudiwa kwa wakati wake ufaao. 7 gNami kwa kusudi hili nimewekwa niwe mhubiri na mtume (nasema kweli katika Kristo wala sisemi uongo), mwalimu wa watu wa Mataifa katika imani na kweli.

8 hNataka kila mahali wanaume wasali wakiinua mikono mitakatifu pasipo hasira wala kugombana.

9 iVivyo hivyo nataka wanawake wajipambe kwa adabu na kwa heshima katika mavazi yanayostahili, si kwa kusuka nywele, kuvalia dhahabu, lulu au mavazi ya gharama kubwa, 10 jbali kwa matendo mazuri kama iwapasavyo wanawake wanaokiri kuwa wanamcha Mungu.

11 kMwanamke na ajifunze kwa utulivu na kwa utiifu wote. 12 lSimpi mwanamke ruhusa ya kufundisha au kuwa na mamlaka juu ya mwanaume. Mwanamke inampasa kukaa kimya. 13 mKwa maana Adamu aliumbwa kwanza, kisha Eva. 14 nWala si Adamu aliyedanganywa, bali ni mwanamke aliyedanganywa akawa mkosaji. 15 oLakini mwanamke ataokolewa kwa kuzaa kwake, kama wakiendelea kudumu katika imani, upendo na utakatifu, pamoja na kuwa na kiasi.

Copyright information for SwhNEN