Isaiah 13

Unabii Dhidi Ya Babeli

1 aNeno kuhusu Babeli ambalo Isaya mwana wa Amozi aliliona:

2 bTwekeni bendera juu ya mlima usio na kitu,
wapazieni sauti,
wapungieni mkono waingie
katika malango ya wenye heshima.
3 cNimewaamuru watakatifu wangu;
nimewaita mashujaa wangu waitimize hasira yangu:
wale wanaoshangilia ushindi wangu.
4 dSikilizeni kelele juu ya milima,
kama ile ya umati mkubwa wa watu!
Sikilizeni, makelele katikati ya falme,
kama mataifa yanayokusanyika pamoja!
Bwana Mwenye Nguvu Zote anakusanya
jeshi kwa ajili ya vita.
5 eWanakuja kutoka nchi za mbali sana,
kutoka miisho ya mbingu,
Bwana na silaha za ghadhabu yake,
kuangamiza nchi yote.

6 fOmbolezeni, kwa maana siku ya Bwana i karibu,
itakuja kama uharibifu kutoka kwa Mwenyezi.
Mwenyezi hapa ina maana ya Shaddai kwa Kiebrania.

7 hKwa sababu ya hili, mikono yote italegea,
moyo wa kila mtu utayeyuka.
8 iHofu itawakamata,
uchungu na maumivu makali yatawashika,
watagaagaa kama mwanamke aliye na utungu wa kuzaa.
Watatazamana kwa hofu kila mtu na mwenzake,
nyuso zao zikiwaka kama moto.

9 jTazameni, siku ya Bwana inakuja,
siku katili, yenye ghadhabu na hasira kali,
kuifanya nchi kuwa ukiwa
na kuwaangamiza wenye dhambi waliomo ndani yake.
10 kNyota za mbinguni na makundi ya nyota
havitatoa mwanga wake.
Jua linalochomoza litatiwa giza
na mwezi hautatoa nuru yake.
11 lNitauadhibu ulimwengu kwa ajili ya uovu wake,
waovu kwa ajili ya dhambi zao.
Nitakomesha majivuno ya wenye kiburi,
na nitakishusha kiburi cha watu wakatili.
12 mNitawafanya wanadamu kuwa adimu kuliko dhahabu safi,
watakuwa wachache sana kuliko dhahabu ya Ofiri.
13 nKwa hiyo nitazifanya mbingu zitetemeke,
nayo dunia itatikisika kutoka mahali pake
katika ghadhabu ya Bwana Mwenye Nguvu Zote,
katika siku ya hasira yake iwakayo.

14 oKama swala awindwaye,
kama kondoo wasio na mchungaji,
kila mmoja atarudi kwa watu wake mwenyewe,
kila mmoja atakimbilia nchi yake ya kuzaliwa.
15 pYeyote atakayetekwa atapasuliwa tumbo,
wote watakaokamatwa watauawa kwa upanga.
16 qWatoto wao wachanga watavunjwa vipande vipande
mbele ya macho yao;
nyumba zao zitatekwa
na wake zao watatendwa jeuri.

17 rTazama, nitawachochea Wamedi dhidi yao,
ambao hawajali fedha
wala hawafurahii dhahabu.
18 sMishale yao itawaangusha vijana,
hawatakuwa na huruma kwa watoto wachanga
wala hawataangalia watoto kwa huruma.
19 tBabeli, johari ya falme,
utukufu wa kiburi cha Wababeli,
Wababeli hapa maana yake ni Wakaldayo.

itaangushwa na Mungu
kama Sodoma na Gomora.
20 vHautakaliwa na watu kamwe
wala watu hawataishi humo kwa vizazi vyote.
Hakuna Mwarabu atakayepiga hema lake huko,
hakuna mchungaji atakayepumzisha makundi yake huko.
21 wLakini viumbe wa jangwani watalala huko,
mbweha watajaza nyumba zake,
bundi wataishi humo
nao mbuzi-mwitu watarukaruka humo.
22 xFisi watalia ndani ya ngome zake,
mbweha ndani ya majumba yake ya kifahari.
Wakati wake umewadia,
na siku zake hazitaongezwa.
Copyright information for SwhNEN