Jeremiah 5:5-6

5 aKwa hiyo nitakwenda kwa viongozi
na kuzungumza nao,
hakika wao wanaijua njia ya Bwana,
sheria ya Mungu wao.”
Lakini kwa nia moja nao pia walikuwa wameivunja nira
na kuvivunja vifungo.
6 bKwa hiyo simba kutoka mwituni atawashambulia,
mbwa mwitu kutoka jangwani atawaangamiza,
chui atawavizia karibu na miji yao,
ili kumrarua vipande vipande yeyote atakayethubutu kutoka nje,
kwa maana maasi yao ni makubwa,
na kukengeuka kwao kumekuwa ni kwingi.
Copyright information for SwhNEN