Job 10

Ayubu: Nayachukia Maisha Yangu

1 a“Nayachukia sana haya maisha yangu;
kwa hiyo nitatoa malalamiko yangu kwa wazi bila kujizuia,
nami nitanena kutokana na uchungu wa moyo wangu.
2 bNitamwambia Mungu: Usinihukumu,
bali niambie una mashtaka gani dhidi yangu.
3 cJe, inakupendeza wewe kunionea,
kuikataa kwa dharau kazi ya mikono yako,
huku wewe ukitabasamu juu ya mipango ya waovu?
4 dJe, wewe una macho ya kimwili?
Je, wewe huona kama mwanadamu aonavyo?
5 eJe, siku zako ni kama zile za mwanadamu,
au miaka yako ni kama ile ya mtu,
6 fili kwamba utafute makosa yangu
na kuichunguza dhambi yangu;
7 gingawa wajua kuwa mimi sina hatia,
na hakuna awezaye kunitoa mkononi mwako?

8 h“Mikono yako ndiyo iliyoniumba na kunifanya.
Je, sasa utageuka na kuniangamiza?
9 iKumbuka kuwa ulinifinyanga kama udongo wa mfinyanzi.
Je, sasa utanifanya kuwa mavumbi tena?
10Je, wewe hukunimimina mimi kama maziwa,
na kunigandisha kama jibini,
11 jukanivika ngozi na nyama,
na kuniunga pamoja kwa mifupa na mishipa?
12 kUmenipa uhai na kunitendea wema,
katika uangalizi wako umeilinda roho yangu.

13 l“Lakini hili ndilo ulilolificha moyoni mwako,
nami ninajua kuwa hili lilikuwa katika nia yako:
14 mKama nilifanya dhambi, ungekuwa umeniona,
wala usingeacha kosa langu lipite bila kuadhibiwa.
15 nKama nina hatia, ole wangu!
Hata kama ningekuwa sina hatia,
siwezi kukiinua kichwa changu,
kwa kuwa nimejawa na aibu,
na kuzama katika mateso yangu.
16 oKama nikiinua kichwa changu juu, unaninyatia kama simba,
na kuonyesha tena uwezo wa kutisha dhidi yangu.
17 pWewe waleta mashahidi wapya dhidi yangu
na kuzidisha hasira yako juu yangu;
nazo nguvu zako zinanijia wimbi moja baada ya jingine.

18 q“Kwa nini basi ulinitoa tumboni?
Ninatamani ningekufa kabla jicho lolote halijaniona.
19 rLaiti nisingekuwako kamwe,
au ningekuwa nimechukuliwa moja kwa moja
kutoka tumboni kwenda kaburini!
20 sJe, siku zangu chache si zimekaribia kuisha?
Niachie ili niweze kupata muda mfupi wa kufurahi
21 tkabla sijaenda mahali ambapo hakuna kurudi tena,
katika nchi ya giza na uvuli wa mauti,
22 unchi ya giza kuu sana,
yenye uvuli wa giza na machafuko,
mahali ambapo hata nuru ni giza.”
Copyright information for SwhNEN