Job 2

Jaribu La Pili La Ayubu

1 aSiku nyingine wana wa Mungu walikuja kujionyesha mbele za Bwana. Shetani naye akaja pamoja nao kujionyesha mbele zake. 2 bBwana akamuuliza Shetani, “Umetoka wapi?”

Shetani akamjibu Bwana “Natoka kuzunguka pote duniani, nikitembea huku na huko humo.”

3 c Bwana akamwambia Shetani, “Je, umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Hakuna mtu mwingine duniani aliye kama yeye, mtu asiye na hatia, ni mnyofu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu. Naye bado anadumisha uadilifu wake, ingawa ulinichochea dhidi yake, ili nimwangamize pasipo sababu.”

4 dShetani akamjibu Bwana, “Ngozi kwa ngozi! Mwanadamu atatoa vyote alivyo navyo kwa ajili ya uhai wake. 5 eLakini nyoosha mkono wako na kuipiga nyama yake na mifupa yake, naye kwa hakika atakulaani mbele za uso wako.”

6 f Bwana akamwambia Shetani, “Vema sana, kwa hiyo, yeye yumo mikononi mwako, lakini lazima umwachie uhai wake.”

7 gBasi Shetani akatoka mbele za Bwana naye akampiga Ayubu kwa majipu mabaya tangu nyayo za miguu yake hadi utosi wa kichwa. 8 hNdipo Ayubu akachukua kigae na kujikuna nacho huku akiketi kwenye majivu.

9 iMke wake akamwambia, “Je, bado unashikamana na uadilifu wako? Mlaani Mungu nawe ukafe!”

10 jAkamjibu, “Unazungumza kama vile ambavyo mwanamke mpumbavu
Mpumbavu hapa ina maana ya kupungukiwa maadili.
yeyote angenena. Je, tupokee mema mikononi mwa Mungu, nasi tusipokee na udhia?”

Katika mambo haya yote, Ayubu hakutenda dhambi katika kusema kwake.

Marafiki Watatu Wa Ayubu

11 lBasi marafiki watatu wa Ayubu, ndio Elifazi Mtemani, na Bildadi Mshuhi na Sofari Mnaamathi, waliposikia juu ya taabu yote iliyompata Ayubu, wakajipanga toka manyumbani mwao, nao wakakutana pamoja kwa makubaliano kwenda kumtuliza katika taabu hiyo na kumfariji. 12 mWalipomwona kwa mbali, ilikuwa vigumu kumtambua. Wakaanza kulia kwa sauti kubwa, wakayararua majoho yao na kujirushia mavumbi juu ya vichwa vyao. 13 nKisha wakaketi chini kwenye udongo pamoja na Ayubu kwa siku saba usiku na mchana. Hakuna yeyote aliyesema naye neno, kwa sababu waliona jinsi mateso yake yalivyokuwa makubwa.

Copyright information for SwhNEN