Job 31

1 a“Nimefanya agano na macho yangu
yasimtazame msichana kwa kumtamani.
2 bKwa kuwa fungu la mwanadamu ni gani kutoka kwa Mungu juu,
urithi wake kutoka kwa Mungu Mwenye Nguvu Aliye juu?
3 cJe, si uharibifu kwa watu waovu,
maangamizi kwa wale watendao mabaya?
4 dJe, yeye hazioni njia zangu
na kuihesabu kila hatua yangu?

5 e“Kama nimeishi katika uongo
au mguu wangu umekimbilia udanganyifu,
6 fMungu na anipime katika mizani za uaminifu,
naye atajua kwamba sina hatia:
7 gkama hatua zangu zimepotoka kutoka kwenye njia,
kama moyo wangu umeongozwa na macho yangu,
au kama mikono yangu imetiwa unajisi,
8 hbasi wengine na wale nilichokipanda,
nayo yale yote niliyootesha na yangʼolewe.

9 i“Kama moyo wangu umeshawishiwa na mwanamke,
au kama nimevizia mlangoni mwa jirani yangu,
10 jbasi mke wangu na asage nafaka ya mwanaume mwingine,
nao wanaume wengine walale naye.
11 kKwa kuwa hilo lingekuwa aibu,
naam, dhambi ya kuhukumiwa.
12 lNi moto uwakao kwa Uharibifu;
Kwa Kiebrania ni Abadon (Ay 26:6; Mit 15:11).

ungekuwa umengʼoa mavuno yangu.

13 n“Kama ningewanyima haki watumishi wangu wanaume au vijakazi wangu,
walipokuwa na manungʼuniko dhidi yangu,
14 onitafanya nini Mungu atakaponikabili?
Nitamjibu nini nitakapoitwa kutoa hesabu?
15 pJe, yeye aliyeniumba tumboni mwa mama yangu,
si ndiye aliwaumba?
Je, si ni yeye huyo mmoja aliyetuumba sote
ndani ya mama zetu?

16 q“Ikiwa nimewanyima maskini haja zao,
au kuyaacha macho ya wajane yadhoofike,
17 rkama nimekula chakula changu mwenyewe,
bila kuwashirikisha yatima;
18 slakini tangu ujana wangu nimemlea yatima kama ambavyo baba angefanya,
nami tangu kuzaliwa kwangu nimewaongoza wajane:
19 tkama nilimwona yeyote akiteseka kwa kukosa nguo,
au mtu mhitaji asiye na mavazi
20 uambaye wala moyo wake haukunibariki
kwa kumpatia joto kwa mavazi ya manyoya ya kondoo zangu,
21 vna kama nimeinua mkono wangu dhidi ya yatima,
nikijua kuwa nina ushawishi mahakamani,
22 wbasi mkono wangu na unyofoke toka begani mwangu,
nao na uvunjike kutoka kiungio chake.
23 xKwa kuwa niliogopa uharibifu kutoka kwa Mungu,
nami kwa kuuogopa utukufu wake sikuweza kufanya mambo kama hayo.

24 y“Kama nimeweka tumaini langu kwenye dhahabu,
au kuiambia dhahabu safi, ‘Wewe ndiwe salama yangu,’
25 zkama nimefurahia wingi wa utajiri wangu,
ustawi ambao mikono yangu ilikuwa imepata,
26 aakama nimelitazama jua katika kungʼaa kwake
au mwezi ukienda kwa fahari yake,
27 abhivyo moyo wangu kushawishiwa kwa siri,
au kubusu mkono wangu kwa kuviheshimu,
28 acbasi hiyo pia ingekuwa dhambi ya kuhukumiwa,
kwa kuwa ningekuwa si mwaminifu kwa Mungu aishiye juu sana.

29 ad“Kama nimeshangilia msiba wa adui yangu,
au kutazama kwa furaha taabu iliyomjia,
30lakini sikuruhusu kinywa changu kufanya dhambi
kwa kuomba laana dhidi ya maisha yake;
31kama watu wa nyumbani mwangu kamwe hawakusema,
‘Ni nani ambaye hajashibishwa na nyama ya Ayubu?’
32 aeLakini hakuna mgeni aliyelala njiani,
kwa maana mlango wangu ulikuwa wazi kwa msafiri;
33 afkama nimeifunika dhambi yangu kama wanadamu wengine wafanyavyo,
kwa kuficha hatia yangu moyoni mwangu,
34 agkwa sababu ya kuogopa umati wa watu,
na hivyo kuwa na hofu ya kudharauliwa na jamaa,
nikanyamaza kimya nisitoke nje ya mlango:

35(“Laiti kama angekuwepo mtu wa kunisikia!
Tazama sasa ninatia sahihi kwenye utetezi wangu:
Mwenyezi na anijibu;
mshtaki wangu na aweke mashtaka yake kwenye maandishi.
36Hakika ningeyavaa begani mwangu,
ningeyavaa kama taji.
37 ahNingempa hesabu ya kila hatua yangu,
ningemwendea kama mwana wa mfalme.)

38 ai“Kama nchi yangu inalia dhidi yangu,
na mifereji yake yote imelowana kwa machozi,
39 ajkama nimekula mazao yake bila malipo,
au kuvunja mioyo ya wapangaji wake,
40 akbasi miiba na iote badala ya ngano,
na magugu badala ya shayiri.”
Mwisho wa maneno ya Ayubu.

Copyright information for SwhNEN