Job 32

Sehemu Ya Tatu: Mazungumzo Ya Elihu

(Ayubu 32–37)

Elihu Awakemea Rafiki Za Ayubu

1 aBasi watu hawa watatu wakaacha kumjibu Ayubu, kwa kuwa alikuwa mwadilifu machoni pake mwenyewe. 2 bLakini Elihu mwana wa Barakeli, wa kabila la Buzi wa jamaa ya Ramu, akamkasirikia sana Ayubu, kwa sababu ya kujihesabia haki mwenyewe badala ya Mungu. 3 cPia aliwakasirikia hao rafiki watatu wa Ayubu, kwa sababu hawakuweza kupata njia ya kuthibitisha ya kuwa hayo maneno ya Ayubu hayakuwa ya kweli, nao bado walikuwa wamemlaumu. 4 dBasi Elihu alikuwa amesubiri kwanza waongee na Ayubu kwa sababu walikuwa na umri mkubwa kumliko yeye. 5Lakini alipoona watu hao watatu hawakuwa na kitu zaidi cha kusema, hasira yake ikaamka.

6 eBasi Elihu mwana wa Barakeli wa kabila la Buzi akasema:

“Mimi ni mdogo kwa umri,
nanyi ni wazee;
ndiyo sababu niliogopa,
sikuthubutu kuwaambia kile ninachojua.
7 fNilifikiri, ‘Yafaa umri useme,
nao wingi wa miaka ungefundisha hekima.’
8 gLakini ni Roho iliyoko ndani ya mwanadamu,
pumzi ya Mwenyezi, ndiyo impayo yeye ufahamu.
9 hSio wazee peke yao walio na hekima,
sio wenye umri mkubwa peke yao wanaofahamu lililo sawa.

10 i“Kwa hiyo nasema: Nisikilizeni mimi;
mimi nami nitawaambia lile ninalojua.
11Nilingojea mlipokuwa mnaongea,
nilizisikiliza hoja zenu;
mlipokuwa mkitafuta maneno ya kusema,
12 jniliwasikiliza kwa makini.
Lakini hakuna hata mmoja wenu
aliyethibitisha kwamba Ayubu amekosa;
hakuna hata mmoja wenu
aliyeweza kujibu hoja zake.
13 kMsiseme, ‘Tumepata hekima;
Mungu na amthibitishe kuwa mwongo,
wala si mwanadamu.’
14 lLakini Ayubu hajayapanga maneno yake dhidi yangu,
nami sitamjibu kwa kutumia hoja zenu.

15 m“Wametiwa hofu na hawana la zaidi la kusema;
maneno yamewaishia.
16Je, ningoje sasa kwa sababu wamekuwa kimya,
kwa vile sasa wanasimama bila kuwa na la kujibu?
17 nMimi nami nitakuwa na la kusema;
mimi nami nitasema lile nilijualo.
18 oKwa kuwa nimejawa na maneno,
nayo Roho iliyomo ndani yangu yanisukuma;
19 pndani yangu niko kama chupa iliyojazwa divai,
kama kiriba kipya cha divai kilicho tayari kupasuka.
20 qNi lazima niseme ili niweze kutulia;
ni lazima nifumbue midomo yangu nipate kujibu.
21 rSitampendelea mtu yeyote,
wala sitajipendekeza kwa mtu yeyote;
22 skwa kuwa kama ningekuwa stadi wa kujipendekeza,
Muumba wangu angeniondolea mbali kwa upesi.
Copyright information for SwhNEN