John 1:19-28

Ushuhuda Wa Yohana Mbatizaji

(Mathayo 3:1-12; Marko 1:1-8; Luka 3:1-18)

19 aHuu ndio ushuhuda wa Yohana wakati Wayahudi walipowatuma makuhani na Walawi kutoka Yerusalemu kumuuliza, “Wewe ni nani?” 20 bYohana alikiri waziwazi pasipo kuficha akasema, “Mimi si Kristo.”
Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta.


21 dWakamuuliza, “Wewe ni nani basi? Je, wewe ni Eliya?”

Yeye akajibu, “Hapana, mimi siye.”

“Je, wewe ni yule Nabii?”

Akajibu, “Hapana.”

22Ndipo wakasema, “Basi tuambie wewe ni nani ili tupate jibu la kuwapelekea wale waliotutuma. Wewe wasemaje juu yako mwenyewe?”

23 eAkawajibu kwa maneno ya nabii Isaya, akisema, “Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani, ‘Yanyoosheni mapito ya Bwana.’ ”

24Basi walikuwa wametumwa watu kutoka kwa Mafarisayo 25 fwakamuuliza, “Kama wewe si Kristo, wala si Eliya na wala si yule Nabii, kwa nini basi unabatiza?”

26 gYohana akawajibu, “Mimi ninabatiza kwa maji,
Hapa tafsiri zingine zinasema ndani ya maji.
lakini katikati yenu yupo mtu msiyemjua.
27 iYeye ajaye baada yangu, sistahili hata kufungua kamba za viatu vyake.”

28 jMambo haya yote yalitukia huko Bethania, ngʼambo ya Mto Yordani, mahali Yohana alipokuwa akibatiza.

Copyright information for SwhNEN