Luke 4:14-15

Mwanzo Wa Huduma Ya Galilaya

(Mathayo 4:12-17; Marko 1:14-15)

14 aKisha Yesu akarudi mpaka Galilaya, akiwa amejaa nguvu za Roho Mtakatifu, nazo habari zake zikaenea katika sehemu zote za nchi za kandokando. 15 bAkaanza kufundisha kwenye masinagogi yao, na kila mmoja akamsifu.

Copyright information for SwhNEN