Matthew 8:1-4

Yesu Amtakasa Mwenye Ukoma

(Marko 1:40-45; Luka 5:12-16)

1Yesu aliposhuka kutoka mlimani, makutano makubwa ya watu yakamfuata. 2 aMtu mmoja mwenye ukoma akaja na kupiga magoti mbele yake, akasema, “Bwana, kama ukitaka, unaweza kunitakasa.”

3Yesu akanyoosha mkono wake akamgusa yule mtu, akamwambia, “Nataka. Takasika!” Mara yule mtu akatakasika ukoma wake. 4 bKisha Yesu akamwambia, “Hakikisha humwambii mtu yeyote. Lakini nenda ukajionyeshe kwa kuhani, na utoe sadaka aliyoamuru Mose, ili kuwa ushuhuda kwao.”

Copyright information for SwhNEN