Psalms 111

Sifa Za Bwana Kwa Matendo Ya Ajabu

1 aMsifuni Bwana.

Nitamtukuza Bwana kwa moyo wangu wote,
katika baraza la wanyofu na katika kusanyiko.

2 bKazi za Bwana ni kuu,
wote wanaopendezwa nazo huzitafakari.
3 cKazi zake zimejaa fahari na utukufu,
haki yake hudumu daima.
4 dAmefanya maajabu yake yakumbukwe,
Bwana ni mwenye neema na huruma.
5 eHuwapa chakula wale wanaomcha,
hulikumbuka agano lake milele.
6 fAmewaonyesha watu wake uwezo wa kazi zake,
akiwapa nchi za mataifa mengine.
7 gKazi za mikono yake ni za uaminifu na haki,
mausia yake yote ni ya kuaminika.
8 hZinadumu milele na milele,
zikifanyika kwa uaminifu na unyofu.
9 iAliwapa watu wake ukombozi,
aliamuru agano lake milele:
jina lake ni takatifu na la kuogopwa.

10 jKumcha Bwana ndicho chanzo cha hekima,
wote wanaozifuata amri zake wana busara.
Sifa zake zadumu milele.
Copyright information for SwhNEN