Psalms 112

Baraka Za Mwenye Haki

1 aMsifuni Bwana.

Heri mtu yule amchaye Bwana,
mtu yule apendezwaye sana na amri zake.

2 bWatoto wake watakuwa wenye uwezo katika nchi,
kizazi cha watu waadilifu kitabarikiwa.
3 cNyumbani mwake kuna mali na utajiri,
haki yake hudumu milele.
4 dHata gizani nuru humzukia mtu mwadilifu,
yule mwenye rehema, huruma na haki.

5 eMema yatamjia mtu yule aliye mkarimu na mwenye kukopesha bila riba,
anayefanya mambo yake kwa haki.
6 fHakika hatatikisika kamwe,
mtu mwenye haki atakumbukwa milele.
7 gHataogopa habari mbaya,
moyo wake ni thabiti, ukimtegemea Bwana.
8 hMoyo wake ni salama, hatakuwa na hofu,
mwishoni ataona ushindi dhidi ya adui zake.
9 iAmetawanya vipawa vyake kwa ukarimu akawapa maskini;
haki yake hudumu milele;
pembe yake itatukuzwa kwa heshima.

10 jMtu mwovu ataona na kuchukizwa,
atasaga meno yake na kutoweka,
kutamani kwa mtu mwovu kutaishia patupu.
Copyright information for SwhNEN