Psalms 113

Kumsifu Bwana Kwa Wema Wake

1 aMsifuni Bwana.

Enyi watumishi wa Bwana msifuni,
lisifuni jina la Bwana.
2 bJina la Bwana na lisifiwe,
sasa na hata milele.
3 cKuanzia mawio ya jua hadi machweo yake,
jina la Bwana linapaswa kusifiwa.

4 d Bwana ametukuka juu ya mataifa yote,
utukufu wake juu ya mbingu.
5 eNi nani aliye kama Bwana Mungu wetu,
Yeye ambaye ameketi juu kwenye kiti cha enzi,
6 fambaye huinama atazame chini
aone mbingu na nchi?

7 gHuwainua maskini kutoka mavumbini,
na kuwanyanyua wahitaji kutoka kwenye jalala,
8 hhuwaketisha pamoja na wakuu,
pamoja na wakuu wa watu wake.
9 iHumjalia mwanamke tasa kutulia nyumbani mwake,
akiwa mama watoto mwenye furaha.

Msifuni Bwana.
Copyright information for SwhNEN