Psalms 132

Maskani Ya Mungu Ya Milele Katika Sayuni

Wimbo wa kwenda juu.

1Ee Bwana, mkumbuke Daudi
na taabu zote alizozistahimili.

2 aAliapa kiapo kwa Bwana
na akaweka nadhiri kwa Yule Mwenye Nguvu wa Yakobo:
3 b“Sitaingia nyumbani mwangu
au kwenda kitandani mwangu:
4 csitaruhusu usingizi katika macho yangu,
wala kope zangu kusinzia,
5 dmpaka nitakapompatia Bwana mahali,
makao kwa ajili ya Yule Mwenye Nguvu wa Yakobo.”

6 eTulisikia habari hii huko Efrathi,
tulikutana nayo katika mashamba ya Yaara:
Yaani Kiriath-Yearimu.

7 g“Twendeni kwenye makao yake,
na tuabudu kwenye kiti cha kuwekea miguu yake;
8 hinuka, Ee Bwana, uje mahali pako pa kupumzikia,
wewe na Sanduku la nguvu zako.
9 iMakuhani wako na wavikwe haki,
watakatifu wako na waimbe kwa furaha.”

10Kwa ajili ya Daudi mtumishi wako,
usimkatae mpakwa mafuta wako.

11 j Bwana alimwapia Daudi kiapo,
kiapo cha uhakika ambacho hatakitangua:
“Nitamweka mmoja wa wazao wako mwenyewe
katika kiti chako cha enzi,
12 kkama wanao watashika Agano langu
na sheria ninazowafundisha,
ndipo wana wao watarithi
kiti chako cha enzi milele na milele.”

13 lKwa maana Bwana ameichagua Sayuni,
amepaonea shauku pawe maskani yake:
14 m“Hapa ni mahali pangu pa kupumzika milele na milele;
hapa ndipo nitakapoketi nikitawala, kwa sababu nimepaonea shauku:
15 nNitambariki kwa kumpa mahitaji tele:
nitashibisha maskini wake kwa chakula.
16 oNitawavika makuhani wake wokovu,
nao watakatifu wake watadumu wakiimba kwa furaha.

17 p“Hapa nitamchipushia Daudi pembe,
Pembe inawakilisha nguvu.

na kuweka taa kwa ajili ya masiya
Masiya yaani mpakwa mafuta.
wangu.
18 sAdui zake nitawavika aibu,
bali taji kichwani pake itangʼaa sana.”
Copyright information for SwhNEN