Psalms 139:7-12


7 aNiende wapi nijiepushe na Roho yako?
Niende wapi niukimbie uso wako?
8 bKama nikienda juu mbinguni, wewe uko huko;
nikifanya vilindi
Vilindi ina maana ya Kuzimu, ambayo ni Sheol kwa Kiebrania.
kuwa kitanda changu,
wewe uko huko.
9Kama nikipanda juu ya mbawa za mapambazuko,
kama nikikaa pande za mbali za bahari,
10 dhata huko mkono wako utaniongoza,
mkono wako wa kuume utanishika kwa uthabiti.

11Kama nikisema, “Hakika giza litanificha
na nuru inayonizunguka iwe usiku,”
12 ehata giza halitakuwa giza kwako,
usiku utangʼaa kama mchana,
kwa kuwa giza ni kama nuru kwako.
Copyright information for SwhNEN