Psalms 26

Maombi Ya Mtu Mwema

Zaburi ya Daudi.

1 aEe Bwana, nithibitishe katika haki,
maana nimeishi maisha yasiyo na lawama;
nimemtumainia Bwana
bila kusitasita.
2 bEe Bwana, unijaribu, unipime,
uuchunguze moyo wangu
na mawazo yangu;
3 ckwa maana upendo wako
uko mbele yangu daima,
nami natembea siku zote
katika kweli yako.
4 d eSiketi pamoja na watu wadanganyifu,
wala siandamani na wanafiki,
5 fninachukia kusanyiko la watenda mabaya
na ninakataa kuketi pamoja na waovu.
6 gNinanawa mikono yangu kwa kuwa sina hatia,
naikaribia madhabahu yako, Ee Bwana,
7 hnikitangaza sifa yako kwa sauti kubwa,
huku nikisimulia matendo yako ya ajabu.
8 iEe Bwana, naipenda nyumba yako mahali unakoishi,
mahali ambapo utukufu wako hukaa.

9 jUsiiondoe nafsi yangu pamoja na watenda dhambi,
wala uhai wangu pamoja na wamwagao damu,
10 kambao mikononi mwao kuna mipango miovu,
ambao mikono yao ya kuume imejaa rushwa.
11 lBali mimi ninaishi maisha yasiyo na lawama;
nikomboe na unihurumie.

12 mMiguu yangu imesimama katika uwanja tambarare;
katika kusanyiko kuu nitamsifu Bwana.
Copyright information for SwhNEN