Psalms 62

Mungu Kimbilio La Pekee

Kwa mwimbishaji. Mtindo wa Yeduthuni. Zaburi ya Daudi.

1 aKwa Mungu peke yake nafsi yangu inapata pumziko;
wokovu wangu watoka kwake.
2 bYeye peke yake ndiye mwamba wangu na wokovu wangu;
yeye ni ngome yangu, sitatikisika kamwe.

3 cMtamshambulia mtu hata lini?
Je, ninyi nyote mtamtupa chini,
ukuta huu ulioinama na uzio huu unaotikisika?
4 dWalikusudia kikamilifu kumwangusha
toka mahali pake pa fahari;
wanafurahia uongo.
Kwa vinywa vyao hubariki,
lakini ndani ya mioyo yao hulaani.

5 eEe nafsi yangu, upumzike, kwa Mungu peke yake,
tumaini langu latoka kwake.
6Yeye peke yake ndiye mwamba wangu na wokovu wangu;
ndiye ngome yangu, sitatikisika.
7 fWokovu wangu na heshima yangu viko kwa Mungu,
ndiye mwamba wangu wenye nguvu
na kimbilio langu.
8 gEnyi watu, mtumainini yeye wakati wote,
miminieni mioyo yenu kwake,
kwa kuwa Mungu ni kimbilio letu.

9 hBinadamu wa ngazi ya chini ni pumzi tu,
nao wa ngazi ya juu ni uongo tu;
wakipimwa kwenye mizani, si chochote;
wote kwa pamoja ni pumzi tu.
10 iUsitumainie vya udhalimu
wala usijivune kwa vitu vya wizi;
ingawa utajiri wako utaongezeka,
usiviwekee moyo wako.

11 jJambo moja Mungu amelisema,
mambo mawili nimeyasikia:
kwamba, Ee Mungu,
wewe una nguvu,
12 kna kwamba, Ee Bwana,
wewe ni mwenye upendo.
Hakika utampa kila mtu thawabu
kwa kadiri ya alivyotenda.
Copyright information for SwhNEN