Psalms 63

Shauku Kwa Ajili Ya Uwepo Wa Mungu

Zaburi ya Daudi. Wakati alipokuwa katika Jangwa la Yuda.

1 aEe Mungu, wewe ni Mungu wangu,
nakutafuta kwa moyo wote;
nafsi yangu inakuonea kiu,
mwili wangu unakuonea wewe shauku,
katika nchi kame na iliyochoka
mahali ambapo hapana maji.

2 bNimekuona katika mahali patakatifu
na kuuona uwezo wako na utukufu wako.
3 cKwa sababu upendo wako ni bora kuliko uhai,
midomo yangu itakuadhimisha.
4 dNitakusifu siku zote za maisha yangu,
na kwa jina lako nitainua mikono yangu.
5 eNafsi yangu itatoshelezwa
kama kwa wingi wa vyakula;
kwa midomo iimbayo
kinywa changu kitakusifu wewe.

6 fKitandani mwangu ninakukumbuka wewe,
ninawaza juu yako makesha yote ya usiku.
7 gKwa sababu wewe ndiwe msaada wangu,
chini ya uvuli wa mbawa zako naimba.
8 hNafsi yangu inaambatana nawe,
mkono wako wa kuume hunishika.

9 iWale wanaotafuta uhai wangu wataharibiwa,
watakwenda chini kwenye vilindi vya dunia.
10 jWatatolewa wafe kwa upanga,
nao watakuwa chakula cha mbweha.

11 kBali mfalme atafurahi katika Mungu,
wale wote waapao kwa jina la Mungu watamsifu,
bali vinywa vya waongo vitanyamazishwa.
Copyright information for SwhNEN