Psalms 70

Kuomba Msaada

(Zaburi 40:13-17)

Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Maombi.

1 aEe Mungu, ufanye haraka kuniokoa;
Ee Bwana, njoo hima unisaidie.
2 bWale wanaotafuta kuuondoa uhai wangu,
waaibishwe na kufadhaishwa;
wote wanaotamani kuangamizwa kwangu,
warudishwe nyuma kwa aibu.
3Wale waniambiao, “Aha! Aha!”
warudi nyuma kwa sababu ya aibu yao.
4 cLakini wote wakutafutao
washangilie na kukufurahia,
wale wapendao wokovu wako siku zote waseme,
“Mungu na atukuzwe!”

5 dLakini bado mimi ni maskini na mhitaji;
Ee Mungu, unijie haraka.
Wewe ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu;
Ee Bwana, usikawie.
Copyright information for SwhNEN